Breaking News

Your Ad Spot

Nov 4, 2016

EU YAWEKEZA EURO MILIONI 1.7 KITUO CHA UTAMADUNI MAKUMIRA

Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer akizungumza katika kituo cha Utamaduni cha Makumira kilichopo mkoani Arusha,mara baada ya kutembelea kituo hicho.(Picha na Ferdinand Shayo).
Meneja mradi huo Randall Stubbs amesema kuwa kwa sasa wanatoa mafunzo ya ngoma za utamaduni wa makabila ya wamasai, wameru na wachaga ikiwa ni pamoja na kufanya maonyesho ya utamaduni katika maeneo mbalimbali.
“Ujenzi utakapokamilika kutakua na ukumbi wa kisasa, jengo maalumu la mafunzo kwa utamaduni wa bara la Afrika, Asia na Ulaya ili utamaduni uweze kuwa endelevu na kurithishwa vizazi na vizazi” alisema Randall.
Meneja Mradi wa Kituo cha Utamaduni cha Makumira, Randall Stubbs akitoa maelekezo kwa Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer alipotembelea kituoni hapo.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer akiwa katika kituo cha Utamaduni cha Makumira kilichopo mkoani Arusha, mara baada ya kutembelea kituo hicho.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa kituo cha utamaduni cha Makumira jijini Arusha.
Meneja Mradi wa Kituo cha Utamaduni cha Makumira, Randall Stubbs akitoa maelezo kwa Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer (kushoto) aliyeambatana na Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama (kulia).
Umoja wa Ulaya (EU) umewekeza zaidi ya Euro milioni 1 na laki 7 katika kituo cha Utamaduni cha Makumira kitengo kilichoko ndani ya Chuo Kikuu cha Makumira ambapo chuo kikubwa cha sanaa kinajengwa pamoja na kumbi ya burudani itakayogharimu kiasi hicho.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) kwa nchi za Afrika Mashariki Roeland Van De Geer amefanya ziara chuoni hapo ambapo amejionea shughuli za ujenzi zinazoendelea katika chuo hicho na kusema kuwa kupitia chuo hicho cha utamaduni wa Tanzania na makabila yake utaendelezwa ili kuleta manufaa kwa vijana na jamii nzima.
Akizungumza na wanahabari mara baada ya ziara hiyo amesema kuwa wataendelea kuunga mkono juhudi za kutunza utamaduni kwani vijana wataweza kutengeneza fursa za ajira kupitia sanaa za utamaduni.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages