Rais Rodrigo Duterte wa Ufilipino amewakosoa
vikali viongozi wa Marekani kutokana na hatua yao ya kusimamisha muamala
wa mauziano ya bunduki elfu 26 kwa nchi yake.
Rais Rodrigo Duterte amesema kuwa, viongozi wa Marekani
waliochukua uamuzi wa usitishaji wa muamala huo ni wapumbavu na tumbili.
Katika hotuba yake hapo jana rais huyo wa Ufilipino aliwatoa wasi wasi
raia wa nchi yake kwamba, kuna uwezekano serikali ya Manila ikaamua
kununua silaha hizo za kijeshi kutoka Uchina au Urusi.
Alisema, "tayari China na Russia zimetualika na ziko tayari kututumia
kiasi chochote cha silaha tunachohitajia." Mwisho wa kunukuu. Jumanne
iliyopita, Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) ilitangaza kusitisha
muamala wa mauziano hayo ya silaha kwa ajili ya polisi ya Ufilipino.
Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilidai kuwa, imechukua hatua hiyo kutokana
na wasi wasi wake juu ya vita dhidi ya magendo ya madawa ya kulevya
vilivyotangazwa na Rais Rodrigo Duterte. Mvutano kati ya Washington na
Manila umezidi kushtadi ambapo hivi karibuni rais wa Ufilipino
alitangaza kukata mahusiano na Marekani.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269