Taasisi ya kupambana na ufisadi wa kifedha
nchini Afrika Kusini imetoa ripoti yake mpya kuhusiana na tuhuma za
ufisadi zinazomkabili Rais Jacob Zuma wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kuna ulazima wa kufanyika uchunguzi
wa kina kuhusiana na suala hilo. Rais Zuma alijitahidi sana kutohusishwa
na ripoti hiyo ya ufisadi wa kifedha, kiasi cha kumfanya wakili wake
wa utetezi kujitoa kunako uamuzi huo. Saa chache baada ya kujiondoa
huko, taasisi ya kupambana na ufisadi wa kifedha nchini humo ilitoa
ripoti yake na hivyo kuchafua zaidi sura ya rais huyo katika fikra za
walio wengi nchini.
Sehemu ya ripoti hiyo yenye kurasa 355 inamuhusisha Rais Jacob Zuma
na ufisadi mkubwa wa kifedha kati yake na familia moja ya Kihindi kwa
jina la Gupta. Inaelezwa kuwa familia hiyo ya wafanyabiashara wa India,
ina taathira kubwa kwenye serikali ya rais huyo, huku ikihusika pia
katika uteuzi wa baadhi ya mawaziri wa serikali yake. Kufuatia ripoti
hiyo, raia wengi wa Afrika Kusini walifanya maandamano hapo jana
wakimtaka Rais Zuma ajiuzulu, ingawa polisi waliingilia kati na
kuwatawanya.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269