.

ZUMA AONDOA KESI YA KUPINGA RIPOTI MAHAKAMANI

Nov 2, 2016

Zuma anakabiliwa na shinikizo za kumtaka ajiuzulu 
 
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesitisha jitihada zake kwa njia ya mahakama, kuzuia kutolewa kwa ripota iliyotengenezwa na aliyekuwa mkuu wa kitengo cha kupambana na rushwa Thuli Madonsela.
Madonsela alifanya uchunguzi kuhusu madai kuwa Zuma aliruhusu familia tajiri ya Gupta kuwa na ushawishi mkubwa serikalini.
Wakili wa bwana Zuma aliiambia mahakama ya juu mjini Pretoria kuhusu uamuzi huo lakini sababu yake bado haijulikani.
Makundi ya upinzani yanafanya maandamano kwenye miji mkubwa nchini Afrika kusini kupinga uongozi wa rais Jacob Zuma.
Image caption Maandamano mjini Pretoria
Maelfu ya watu wako mji mkuu Pretoria wakimtaka Zuma ajiuzulu. Ripoti hiyo inaaminiwa kuwa na lawama za kumharibia jina bwana Zuma.
Hatua ya Zuma ya kuzuia kutolewa kwa ripoti hiyo zilipingwa na vyama vya upinzani ambavyo sasa vinataka alipie gharama ya kesi.
Bado haibainiki ni lini ripoti hiyo ilitolewa rasmi kwa umma. Bwana zuma amekumbwa na madai yanayohusu ufisadi kwa zaidi ya miaka kumi.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª