Matatizo yote ya kiusalama yaliyopo hivi sasa katika eneo nyeti la Mashariki ya Kati yanatokana na tangazo la Balfour.
Miaka 99 iliyopita, dola la
kikoloni la Uingereza ilitoa tangazo la Balfour tarehe pili Novemba
1917. Arthur James Balfour, ndiye aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa
Uingereza wakati huo. Balfour alisoma tangazo hilo mbele ya Baron
Walter Rothschild mkuu wa jamii ya Mayahudi wa Uingereza aliyekuwa pia
mbunge wa nchi hiyio. Tangazo la Balfour lilikuwa na nafasi kubwa katika
kuasisiwa mfumo maalumu wa kiusalama kwenye eneo la magharibi mwa
Asia.
Tangazo hilo lilikuwa batili tangu siku
yake ya mwanzo kabisa kwani serikali ya Uingereza ililitumia kuasisi
dola pandikizi la Kizayuni linaloitwa Israel katika ardhi ya nchi
nyingine wakati hakuna sheria yoyote iliyoipa haki hiyo. Tangazo hilo
ndio uliokuwa msingi wa kuundwa Israel mwaka 1948 katika ardhi za
Palestina zinazokaliwa kwa mabavu hadi leo hii, na tangu wakati huo,
ukaanza mgogoro wa Palestina na eneo zima la Mashariki ya Kati bali
ulimwengu mzima wa Kiislamu. Hadi hivi sasa mgogoro huo uliotokana na
tangazo la mwezi Novemba 1917 la Balfour umeshasababisha vita
visivyopungua vinane baina ya Israel na nchi za Karabu. Vita vingi zaidi
kati ya hivyo ni vile vilivyotokea baina ya Israel na Lebanon na Israel
na Palestina. Vita vya miaka ya 1948, 1956, 1967, 1972, 2006, 2008,
2012 na vita vya mwaka juzi 2014 ni miongoni mwa vita vikubwa zaidi
vilivyotokea baina ya utawala pandikizi wa Israel na nchi za Kiarabu.
Fauka ya hayo, hadi hivi sasa Israel
imeshafanya makumi ya mashambulizi ya muda mfupi na ya hapa na pale
dhidi ya Lebanon na dhidi ya maeneo machache yaliyobakia mikononi mwa
Wapalestina, kama ambavyo kumeshafanyika Intifadha tatu hadi hivi sasa
za kupambana na Wazayuni. Intifadha ya kwanza ni ile iliyoanza mwaka
1978 na kumalizika mwaka 1993, yaani baada ya miaka 15 ya kuanza kwake.
Intifadha ya pili ilianza mwaka 2000 na kuendelea hadi mwaka 2005, na
Itifadha ya tatu ya Wapalestina ilianza mwezi Oktoba mwaka jana 2015 na
ingali inaendelea hadi hivi sasa.
Matokeo ya mashambulizi, vita na
Intifadha zote hizo ni kuuawa na kujeruhiwa pamoja na kuwa wakimbizi
mamilioni ya raia Waarabu, nje na ndani ya ardhi za Palestina. Matokeo
ya jambo hilo ni kuongezeka umaskini, ukosefu wa kazi, ukosefu wa
utulivu na majanga mengine mengi katika eneo hili la magharibi mwa Asia.
Zaidi ya hayo, Israel ndiyo nembo kuu ya
ugaidi wa kiserikali na imekuwa ikiua watu muhimu wa ulimwengu wa
Kiislamu katika maeneo tofauti duniani. Utawala wa Kizayuni wa Israel
ndiyo sababu kuu ya uingilia wa madola ya Magharibi katika masuala ya
ndani ya nchi za eneo hili. Ni jambo lisilo na shaka kuwa, uingiliaji wa
mambo ya ndani ya nchi nyingine ni miongoni mwa mambo yanayoongeza
ukosefu wa amani na utulivu na kuzusha mizozo baina ya nchi za eneo
husika. Si hayo tu, lakini pia utawala wa Kizayuni wa Israel ni moja ya
wavunjaji wakuu wa haki za binadamu duniani.
Utawala ambao unapora maeneo ya
Wapalestina na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni. Bila ya shaka
ni kwa kuzingatia hali hiyo ndio maana tunaweza kusema kuwa, Tangazo la
Balfour ndilo chimbuko na chanzo cha ukosefu wa amani na usalama katika
eneo la Mashariki ya Kati, na kwa mara nyingine tena, mkoloni kizee
Uingereza, ndiye muhusika wa mabalaa na majakamoyo yote haya.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269