TAARIFA YA KUSIKITISHA KUTOKA KATA YA MASANZE JIMBO LA MIKUMI.
OFISI YA
MBUNGE Jimbo La Mikumi inalaani sana kitendo cha kinyama kilichofanywa
na Ndugu zetu wa jamii ya wafugaji kwa kujichukulia sheria mkononi na
kumjeruhi vibaya Ndugu Augustino Mtitu mkulima wa kitongoji cha
Upangwani, Kijiji cha Dodoma Isanga, Kata Ya Masanze Jimbo la Mikumi
ambapo jana 25 desemba majira ya Mchana amechomwa mkuki mdomoni na
kutokezea nyuma ya shingo yake, ambapo alipelekwa hospitali ya wilayani
Kilosa na baadae amekimbizwa hospitali ya mkoa Morogoro ili kufanyiwa
operesheni ya kuondoa mkuki huo na kwa matibabu zaidi.
Augustino
Mtitu alishambuliwa na wafugaji wa kimasai alipokuwa akimsaidia jirani
yake kufukuza Ng’ombe wasiharibu mazao shambani kwake,
Kipande
cha mti kinachoonekana hapo mdomoni ndiyo mkuki uliokatwa ili kupunguza
urefu wa mkuki huo wakati wakimkimbiza hospitali, Inasemekana MwenyeKiti
wa kijiji na MwenyeKiti wa kitongoji hicho nao wamejeruhiwa.
WITO KWA SERIKALI.
Ofisi Ya
Mbunge Mikumi inatoa wito kwa Serikali kuwabaini wale wote waliofanya
kitendo hiki cha kinyama kuhakikisha wanachukuliwa hatua kali za
kisheria ili kuweza kukomesha vitendo hivi vya kujichukulia sheria
mkononi inayopelekea kuongezeka kwa uvunjifu mkubwa wa Amani na migogoro
isiyokwisha kati ya wakulima na wafugaji wilayani KILOSA.
Imetolewa na:-
Robert A. Galamona
Katibu Ofisi Ya Mbunge
Mikumi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269