Breaking News

Your Ad Spot

Dec 8, 2011

VODACOM- M PESA YAUNGANA NA WESTERN UNION

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom (T) Rene Meza akizungumza
wakati wa uzinduzi wa huduma hizo pacha, jiji Dar es Salaam
Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imepanua zaidi huduma zake za M PESA kwa kuunganisha huduma hiyo na huduma ya kimataifa ya kutuma na kupokea fedha Western Union.

Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hiyo, leo mjini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Rene Meza alisema sasa wateja wa M PESA wanaweza kutumiwa fedha kupitia huduma ya Western Union kutoka zaidi ya nchi 65 zenye mtandao wa huduma hiyo.

"Siku zote Vodacom hutafuta suluhisho la mahitaji ya wateja wake kupitia huduma bunifu kama hii ambayo tunazindua leo", alisema Rene katika uzinduzi huo uliofanyika hoteli ya Hyatt Regeny.

Alisema Vodacom imeamua kuugnanisha huduma zake na West Union kufuatia kuwepo kilio cha muda mrefu kwa wateja kutaka huduma ya M PESA ivuke mipaka.

Meza alisema kuanzia jana huduma hiyo imeanza  hivyo wateja wa M PESA wanaweza kupokea fedha kutoka kwa ndigu au jamaa zao wanaoishi nchi za nje zikiwemo Kenya na Uganda na hakuna gharama za ziada zaidi ya zile za kawaida  kuchukua fedha kutoka kwa wakala wa M PESA.

Alisema huduma ya Vodacom-M PESA iliyozinduliwa mwaka 2008 sasa inao wateja zaidi ya milioni tisa ikifanya miamala zaidi ya milioni moja kwa siku, ikiwa ni huduma ambazo mbali na kutuma na kupokea fedha pia huwezesha mteja kulipia huduma mbalimbali kama  za maji,umeme, kuongeza salio,kulipa kodi na kununua tiketi za ndege.

Naye Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Western Union, Karen Jordaan alisema kwa huduma hiyo ni kwa wateja wa M PESA kupokea fedha tu na siyo kutuma.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages