Mwanachama
wa chama cha siasa cha TLP Bwn Macmillan Lyimo (kushoto) akirejesha
fomu ya kuomba kugombea uraisi kwa tiketi ya chama hicho kwa katibu mkuu
wa chama hicho Meja Jesse Makundi huku katibu msaidizi wa TLP Bwn Hamad
Tao akishuhudia.Picha ilipigwa mwaka 2010 kwa hisani ya http://changamotoyetu.blogspot.com
………………………………………………………………………….
Na Happy Shirima-MAELEZO-
Dar es salaam Mwanachama
wa chama cha Tanzania Labour Party [TLP] Macmillan Lyimo ametangaza nia
ya kugombea nafasi ya uraisi kupitia chama hicho.
Lyimo ametangaza azma hiyo leo jijini Dar es salaam wakati
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu nia yake ya kuamua kugombea
urais kupitia Chama hicho na sababu zilizo mfanya agombee
Amesema kuwa sababu zilizomfanya agombee nafasi hiyo kupitia
chama hicho ni kuendeleza juhudi za Mwenyekiti wa chama hicho Mhe.
Augustino Mrema za kutunza historia nzuri alioiweka kwenye chama hicho
wakati wa uchaguzi wa mwaka 1995.
”Mhe.Mrema ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa chama na Mbunge wa
Jimbo la Vunjo itakuwa ni aibu na fedheha kwa mtu yeyote kutotambua
mchango wa kiongozi huyo wakati akiwa kiongozi serikalini na hatimaye
wakati akiwa upinzani toka 1995 ”alisema Lyimo.
Aidha amesema kuwa sera kuu ya chama hicho ni amani , kuandaa
kizazi kipya na taifa jipya Tanzani litakalo jengwa na misingi mkuu
ukiwa ni Mungu kupewa nafasi ya kwanza lengo kuu ikiwa ni kuifanya
Tanzania kuwa taifa kubwa la dunia katika kipindi kifupi.
Ametoa wito kwa viongozi wa kada zote na wananchi wote kushiriki
kwa amani na upendo katika matukio makuu muhimu kwa Taifa hilo ambayo
ni kupigia kura Katiba inayopendekezwa ,uchaguzi mkuu na kujenga umoja
ili kuepuka ufa uliojitokeza katika masuala ya dini kwa ajili ya
mustakabali mzuri wa Tanzania .
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269