Breaking News

Your Ad Spot

Feb 12, 2015

MASHEHA WILAYA YA MICHEWENI PEMBA WATAKIWA KUTOUZA ARDHI BILA KUIARIFU SERIKALI

indexNa Masanja Mabula -Pemba .
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Jabu Khamis Mbwana amewataka masheha kutoingia mikataba ya uuzaji au utoaji wa ardhi katika maeneo yao  bila ya kuiarifu Serikali ya Wilaya lengo ni kuzuia migogoro ya ardhi .
Akizungumza na masheha wa Wilaya hiyo huko Ofisini kwake Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa iwapo masheha watajiepusha na mikataba hiyo migogoro ya ardhi ambayo inaikabili jamii inaweza kupungua .
Amefahamisha kwamba ni kosa kwa Sheha kujichujkulia uwamuzi wa kuingia mkataba wa kuuza ardhi na kufahamisha kuwa Serikali ya Wilaya haitokuwa tayari kumvulia Sheha ambaye atasababisha mgogoro kwa kuingia mtakaba ya aina hiyo .
“Ili kujiepusha na migogoro ya ardhi katika shehia zenu , jiepusheni kuingia mikataba ya kuuza au kutoa ardhi na kwa ahili Serikali ya Wilaya haitakuwa kubeba mzigo kwa kumtetea sheha atakayesababisha mgogoro ya ardhi ” alifahamisha .
Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka masheha katika Wilaya hiyo kufanya kazi kwa mujibu wa sharia na kuhakikisha kwamba wanawatumikia wananchi wote bila ya kujali itikadi za vyama , rangi , dini wala kabila .
Amesema kuwa sheha anajukumu la kutenmda haki kwa wananchi katika shehai yake na kuwasisitiza kutumia lugha ya hekima na busara wakati wanapo watumukia wananchi ili kujenga imani na matumani kwa raia na Serikali yao .
“Fanyeni Haki  na Uadilifu kwa wananchi wote katika shehia zenu , pia tumieni lugha za hekima na busara wakati mnapotoa huduma na hii itawafanya wananchi waongeze imani na matumani kwa Serikali yao ” alieleza Jabu .
Naye Afisa Tawala wa Wilaya hiyo Ahmed Khalid Abdalla amesema kuwa ni vyema masheha kuwasiliana na Ofisi ya Wilaya ili kupata maelekezo yanayofaa na kuacha kukurupuka kuingia mikataba ambayo inakuwa na athari kwa siku za baadaye .
“Acheni kukurupuka kuingia mikataba , ni vyema mkawasiliana na Ofisi ya Wilaya ili kupata maelekezo sahihi ambapo kwa kufanya hivyo kutazuia kutokea migogoro ya ardhi katika Shehia zenu ” alisisitiza Ahmed .
Akiizungumzia hotuba hiyo Sheha wa Shehia ya Mihogoni Salim Said amewataka masheha kuwa waadilifu kwa kujiepusha na vitendo ambavyo zinaweza kusababisha migogoro ikiwemo masuala ya uuzaji wa Ardhi hasa za mashamba ya Serikali .

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages