Breaking News

Your Ad Spot

Feb 12, 2015

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

index
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MHAMIAJI HARAMU MMOJA RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MEKESA ABADA (27) KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI. AIDHA MHAMIAJI HUYO ALIKUWA PAMOJA NA MWENYEJI WAKE AITWAYE ADIKO MICHAEL (32) MKAZI WA MWANJELWA AMBAYE NAE AMEKAMATWA.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 11.02.2015 MAJIRA YA SAA 22:30 USIKU HUKO KATIKA ENEO LA BARABARA YA SITA, SOKOMATOLA, KATA NA TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA. KATIKA MSAKO WA PILI:
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA MAKONGOLOSI WILAYANI CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JUMA JUMA (18) ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI MSOKOTO MMOJA SAWA NA UZITO WA GRAM 05.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 11.02.2015 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA MAKONGOLOSI, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA BAADA YA KUFANYIKA MSAKO KATIKA MAENEO HAYO. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA VITENDO VYA KUSHIRIKI KUWAINGIA RAIA WA KIGENI NCHINI BILA KUFUATA TARATIBU KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWAO. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII/VIJANA KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. Imesainiwa na: [AHMED Z. MSANGI – SACP] KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages