Mkurugenzi
Mkuu wa TBL Group ,Roberto Jarrin akisisitiza jambo kwa waandishi wa
habari , wakati lipokuwa akitoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni
hiyo kwa kipindi cha mwaka jana na kutangaza mikakati ya mwaka
huu,mkutano huo ulifanyika makao makuu ya kampuni hiyo Ilala jijini
Dar es Salaam leo Mei 26,2016.
Mkurugenzi
Mkuu wa TBL Group ,Roberto Jarrin akisisitiza jambo kwa waandishi wa
habari , wakati lipokuwa akitoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni
hiyo kwa kipindi cha mwaka jana na kutangaza mikakati ya mwaka
huu,mkutano huo ulifanyika makao makuu ya kampuni hiyo Ilala jijini
Dar es Salaam
Mwandishi
wa gazeti la The East Africa Kidanka Christopher akiuliza swali kwa
Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group ,Roberto Jarrin (hayupo pichani) kuhusiana
na uzalishaji wa pombe za asili , wakati wa mkutano na wandishi wa
habari wa kutoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni hiyo kwa kipindi
cha mwaka jana na kutangaza mikakati ya mwaka huu,mkutano huo
ulifanyika makao makuu ya kampuni hiyo Ilala jijini Dar es Salaam
Baadhi
ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliohudhuria katika
mkutano wa TBL Group , wa kutoa tathmini ya utendaji kazi wa kampuni
hiyo wakimsikiza kwa makini, Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group ,Roberto
Jarrin (hayupo pichni) wakati wa mkutano huo ulifanyika makao makuu ya
kampuni hiyo Ilala jijini Dar es Salaam
Mtalamu
wa upishi wa vinywaji wa TBL Group (Techincal Brewer) Emanuel Sawa
akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya bia aina ya Castle Luger, jinsi
inavyozalishwa wakati walipotembelea kiwanda hicho mara baada ya
kumalizika kwa mkutano wa tathmini na waandishi hao
……………………………………………………………………………………………..
Kampuni ya TBL Group imelipa kodi ya mapato ya kiasi cha shilingi bilioni 81 katika kipindi cha mwaka 2015.
Akitoa taarifa ya tathmini ya
utendaji wa kampuni ya mwaka uliopita kwa waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam leo,Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group Roberto Jarrin pia
amebainisha kuwa mbali na kampuni kulipa kiasi hicho cha kodi pia
imekusanya kodi za serikali kiasi cha shilingi bilioni165 ikiwa ni kodi
ya mlaji (exercise duty) ,bilioni 114 ikiwa ni kodi ya ongezeko la
thamani (VAT) na bilioni 24 ikiwa ni malipo ya kodi nyinginezo ikiwemo
kodi ya PAYE.
TBL Group ni kampuni inayoongoza
kulipa kodi nchini ikiwa imechagia pato la serikali kwa njia ya kodi
kiasi cha shilingi Trilioni 2.3 katika kipindi cha miaka 10 “Kampuni
yetu imechangia maendeleo ya taifa kwa njia ya kukusanya na kulipa kodi
na mchango huo umekuwa ukitambuliwa na taasisi mbalimbali na kuitunukia
tuzo ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambayo imeitunukia tuzo
ya Mlipa kodi bora nchini kwa kipindi cha miaka mine mfululizo”.Alisema Jarrin.
TBL Group inajumuisha makampuni
ya- Tanzania Breweries Limited (TBL), Tanzania Distilleries Limited
(TDL) na Dar Brew Limited.Biashara kuu ya kampuni ni kuzalisha na
kuuza vinywaji ikiwemo bia za aina mbalimbali,vinywaji vikali na
vinywaji vya asili..
Jarrin alibainisha hayo wakati
akitoa ripoti ya utendaji wa kampuni katika kipindi cha mwaka 2015 na
mikakati yake ya mbele katika kipindi cha mwaka 2016/17 kwa waandishi wa
habari “TBL Group itaendelea kuunga jitihada za serikali zakukuza
sekta ya viwanda nchini kwa kuendelea kujenga viwanda nchini na tangu
kampuni hiyo ibinafsishwe mwaka 1994,imekuwa ikiendelea kuwekeza na
tayari imewekeza Zaidi ya shilingi bilioni 150 kwa ajili ya kujenga
viwanda vilivyokuwepo awali uwa vya kisasa Zaidi kuendana a teknolojia
ya kisasa”
Kampuni inavyo viwanda 10 nchini
na miongoni wa viwanda vyake vilivyopo katika mikoa ya Mwanza,Mbeya na
Dar es Salaam vimetunukiwa tuzo mfululizo za kuwa viwanda bora katika
viwanda vinavyomilikiwa a kampuni mama ya SABMiller katika bara la
Afrika.TBL Mwanza na Mbeya vikiwa katika kundi la viwanda 10 na 15 kwa
ubora duniani.
Jarrin alisema biashara ya bia za kampuni ya TBL zinatawala soko kwa asilimia 78 nchini ikiwa inaongozwa na aina za bia za Safari, Kilimanjaro, Ndovu, Castle lager na Castle Lite .Pia kampuni inatengeneza mvinyo na vinywaji vikali maarufu vinavyotamba kwenye soko kwa asilimia 73 ambavyo ni – Konyagi, Valuer and Dodoma Wine – Kwa upande wa vinywaji vya asili vinywaji vyake vinatawala soko kwa asilimia 8 ambavyo ni – Chibuku and Nzagamba
– Utafiti uliofanywa na taasisi ya CanBack kuhusiana na matumizi ya
pombe za asili nchini umebainisha kuwa matumizi ya pombe za asili nchini
ni asilimia 50%
Jarrin aliendelea kueleza kuwa
TBL Group inaendelea kutoa mchango wa kukuza uchumi wa taifa kupitia
katika sekta ya uuzaji vinywaji ambayo imetoa ajira zaidi ya milioni 2
za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja zinazoendelea kuwanufaisha
watanzania wa kada mbalimbali.Kwa upande wa sekta ya kilimo wakulima wa
zao la Shahiri Zaidi ya 3000 wamenufaika kupitia mpango wa kushirikiana
na kampuni.Katika kipindi cha mwaka 2015 mpango huu umewezesha ongezeko
la uzalishaji wa zao hilo kufikia tani 15,574 kiasi ambacho kimevuka
lengo la matumizi na mahitaji ya kampuni.
Pia imebainishwa kuwa zaidi ya
wakulima 700 wananufaika na mpango wa kiwanda cha TDL wa kushirikiana
nao atika kilimo cha zabibu kinachoendeshwa katika vijiji vya Bihawana,
Mpunguzi,, Mvumi, Hombolo, Mbabala, Veyula, Makang’wa, Mzakwe na
Mbalawala .Chini ya mpango huo wakulima wanawezeshwa kupatiwa utaalamu
wa kilimo kwa kushirikiana na taasisi ya Makutupora Viticulture Training
and Research Center (MVTRC). Pia chini ya mpango huu watoto wa wakulima
wa zao la zabibu wamekuwa wakisaidiwa kielimu kupitia mfuko
unaojulikana kama Zabibu na Shule Kwanza.
Jarrin pia alibainisha kuwa
kampuni ya DarBrew imeweza kuleta mapinduzi ya uuzaji wa pombe za asili
nchini kwa kuwawezesha watumiaji kupata kinywaji cha Chibuku na Nzagamba
kikiwa kimefungwa kwa viwango mbalimbali na katika mazingira ya usafi
yanayolinda afya za watumiaji na hivi sasa imekuja na mkakati wa
kuwainua akina mama kimapato kupitia kuuza bidhaa zake unaojulikana kama
Chibuku Mamas ambao hadi kufikia sasa wanawake wapatao 130
wameishajiunga na mpango huu.
Kuhusu mtazamo wake wa hali ya
biashara ya kampuni kwa sasa Jarrin alisema sekta ya uuzaji wa vinywaji
inakabiliwa na changamoto mbalimbali mojawapo ni bei kubwa ya bia ambayo
watumiaji wake wengi wanashindwa kuimudu,kuwepo na vinywaji visivyo
katika mfumo rasmi wa ushindani katika soko,kukosekana kwa motisha
katika uzalishaji wa malighafi za kutengeneza vinywaji nchini kwa kuwa
zinatozwa kodi kubwa ya zuio kuliko malighafi zinazotolewa nje ya nchi.
Alisema baadhi ya mambo
yanayostahili kufanyika katika uboreshaji wa sekta ili iendelee
kuchangia pato la taifa ni kupunguza kodi za malighafi zinazozalishwa
nchini kama kimea kinachotumika kutengeneza bia pia kulasimisha pombe za
asili ziende sambamba na vinywaji vya sili vinavyolipiwa kodi na
kuhakikisha vinywaji vya asili vinapatikana katika mazingira ya usafi “Pamoja
na changamoto nyingi zilizopo katika sekta hii tunaendelea kukabiliana
nazo na tumedhihirisha uwezo wetu kwa kuwa na viwanda vyenye ubora wa
hali ya juu nchini Tanzania”Alisema Jarrin
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269