Mkuu
wa Kitengo cha Burudani na Digitali wa Tigo, Paulina Shao (kushoto),
akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
kuhusu tamasha la nyama choma litakalofanyika Viwanja
vya Leaders kesho kutwa Jumamosi Mei 28, 2016 jijini Dar es Salaam,
ambapo mwanamuziki Ben Pol atatoa burudani kwa udhamini wa kampuni ya
Tigo. Kulia ni Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo, Carol Ndosi na katikati ni
mwanamuziki Ben Pol.
Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo, Carol Ndosi (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Mwanamuziki, Ben Pol (katikati), akizungumza katika mkutano huo.
Mtaalamu wa Kidigitali, Samira Baamar (kushoto), akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
Kampuni
inayooongoza kwa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania leo imekubali
kumdhamini mwanamuziki nguli na mtunzi wa nyimbo za muziki, Bernard
Michael Paul Mnyang'anga, maarufu kama ‘Ben Pol’ kuburudisha katika
tamasha la mwaka huu la Nyama Choma.
Tamasha
hilo ambalo linafanyika kwa mwaka wa tano sasa ni moja ya tamasha
maarufu linalovutia watu wengi kutoka maeneo yote ya Dar es Salaam
litafanyika kwenye viwanja vya Leaders Jumamosi Mei 28, 2016.
Akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari, Mkuu wa Tigo wa masuala ya
Dijitali Paulina Shao alisema kuwa kumuunga mkono Ben Pol kunaonesha
kuendelea kujikita kwa Tigo katika kuwekeza katika kusaidia sekta ya
muziki ya ndani kwa kuhakikisha wasanii wanawezeshwa kufikia viwango
vya juu katika kazi zao.
“Kama
kampuni ya maisha ya kidijitali, Tigo inatambua mchango muhimu wa
wasanii wa Tanzania wanaoutoa katika sekta ya burudani.
Hii
ndio maana tumewekeza kwa kiwango kikubwa kuwasaidia wasanii
hususani wanamuziki wa ndani katika kuhakikisha wanafahamika katika
masoko ndani ya nchi, kikanda na kimataifa kwa kutumia majukwaa ya
kidijitali yanayokuwepo na kushiriki matukio mbalimbali na hivyo
kuongeza mauzo ya muziki wao pamoja na nembo zao,” alisema Shao.
Aidha
akiishukuru Tigo kwa uungwaji mkono huo, Ben Pol aliisifu Tigo kwa
juhudi inazofanya bila kuchoka katika kukuza ukuaji wa sekta ya
muziki wa ndani kupitia Jukwaa la Muziki la Tigo.
“Ninaishukuru
sana Tigo kwa uungwaji mkono ambao ni muendelezo wa mtiririko wa
programu ambazo imezianzisha ili kuinua maisha ya wasanii wachanga wa
Tanzania,” alisema Ben Pol na kutoa changamoto kwa wasanii wanaoibukia
kuwa wasione aibu kuomba msaada kutoka kwa mashirika kama Tigo.
Nguli huyo wa muziki wa Bongo Flava kwa hivi sasa anatamba na kibao ‘MoyoMashine’ ambayo aliitoka hivi karibuni.
Ben
Pol ni miongoni mwa wasanii wanaonufaika na jukwaa la Muziki la Tigo
ambalo lilianzishwa mwaka 2015 likiwa na lengo la kuiunga mkono sekta
ya muziki Tanzania kwa kuwasaidia wasanii wa ndani kupata kipato zaidi
kutokana na mauzo ya kazi zao na kuwawezesha kufahamika katika masoko
ya kimataifa kupitia majukwaa hayo ya kidijitali kama vile Music
portal na Deezer, ambayo ni majukwaa ya kimataifa yaliyo kwenye mtandao
yakiwa na nyimbo kutoka sehemu mbalimbali duniani zaidi ya milioni
36.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269