Kansela Angela Merkel wa Ujerumanin Jumamosi Feb 25, 2017 awashutumu washirika wake katika serikali ya mseto kwa
kupendekeza marekebisho kwa magaeuzi ya ustawi wa jamii.
Kansela Angela Merkel wa Ujerumanin Jumamosi Feb 25, 2017 awashutumu
washirika wake katika serikali ya mseto kwa kupendekeza marekebisho kwa
magaeuzi ya ustawi wa jamii ambayo yanapongezwa kwa kuchochea mafanikio
ya uchumi wa taifa.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni mgombea wa
chama cha SPD amempiku Merkel wakati nchi ikielekea katika uchaguzi mkuu
uliopangwa kufanyika mwezi wa Septemba mwaka huu. Chama hicho kwa miaka
kadhaa kilikuwa nyuma ya muungano wa wahafidhina wa Merkel katika
uchunguzi wa maoni. Lakini kuungwa mkono kwa chama hicho cha sera za
wastani mrengo wa kushoto kumeongezeka tokea kilipomteuwa spika wa
zamani wa bunge la Ulaya kuwa mgombea wao mwishoni mwa mwezi wa Januari.
Martin
Schulz alitaka kuuvutia upande wa sera za mrengo wa kushoto wa chama
chake hapo Jumatatu kwa kusema marekebisho yanahitajika kwa mageuzi ya
"Agenda 2020"
ambayo yaliandaliwa na Kansela Gerhard Schroeder wa chama cha SPD lakini ikamghariu wadhifa wake huo na kukigawa chama.
Mageuzi
hayo yaliyozinduliwa mwaka 2013 yalisababisha wanachama wengi wa SPD
kujitowa na kujiunga na chama cha sera kali za mrengo wa kushoto Die
Linke.
Mpango wa mageuzi wasifiwa
Kansela
Angela Merkel akiwa katika jimbo lake la uchaguzi la Stralsund na
kiongozi wa wabunge wa CDU Vincent Kokert katika bunge la jimbo la
Mecklenburg-Western Pomerania.
Lakini Merkel ameusifu
mpango huo wa mageuzi katika kampeni ya uchaguzi kwenye jimbo lake la
uchaguzi la Sraklsund kaskazini mwa Ujerumani Jumamosi kwa kusema "Ndio
maana nilisema wakati nilipoingia madaraka miaka 11 iliopita kwamba
Kansela Schroeder ametowa mchango mkubwa kwa Ujerumani kwa agenda yake
hiyo ya 2010.
Amesema wahafidhina wamefanya baadhi ya marekebisho
ya mageuzi tokea mwaka 2005 wakati walipounda serikali ya mseto lakini
ilishikilia kiini cha mpango huo kwa sababu uliwapatia ajira watu wengi
na kiwango cha watu wasiokuwa na kazi kikapunguwa kwa nusu tokea mwaka
2005.
Merkel amesema lakini siku hizi chama cha SPD hakitaki
kuutangaza mpango huo kuwa ni wa mafanikio.Amesema Ujerumani inahitaji
kuwa na mdahalo kuhusu Agenda 2025 na amekituhumu chama cha SPD kwa
kuendelea kuangalia kipindi chake kilichopita na sio mustakbali wake.
Pia
amesema ni muhimu kuiandaa Ujerumani kwa mabadiliko makubwa kupitia
utandawazi na kutowa wito kwa makampuni yanayotumia fedha kwa ajili ya
utafiti yapunguziwe kodi ili kuzishajiisha kampuni ndogo ndogo zifanye
utafiti zaidi.
Malipo ya uzeeni yatetewa
Martin Schultz kiongozi wa chama cha SPD na mgombea ukansela kwa tiketi ya chama hicho.
Katika
hotuba yake hapo Jumatatu Schulz alizungumzia juu ya kuwahami
wafanyakazi wazee pamoja na kuanzisha vikwazo kwa mikataba ya kazi ya
muda na kutetea malipo ya uzeeni.
Waajiri wanasema jambo hilo litaumiza uchumi.
Schulz
ameiambia kampuni ya vyombo vya habari Redaktionsnetzwerk Deutchland
(RND) kwamba anataraji uchaguzi wa Septemba 24 utakuwa wa mchuano
mkali.
Schulz amesema zaidi ya asilimia 20 ya wapiga kura
huaumuwa siku kumi za mwisho wakati asilimia mbili hadi tatu huamuwa
siku ya uchaguzi yenyewe na kwamba matokeo huenda yakategemea asili hiyo
mbili au tatu ya siku ya mwisho
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269