Enles Mbegalo
WAZIRI wa Kilimo ,Chakula,Mifugo na Uvuvi Dk. Charles Tizeba
(pichani), anatarajia kufungua kongamano la siku tatu la wadau wa sera
za kilimo kesho jijini Dar es Salaam.
Aidha, kongamano hilo litahudhuriwa na wadau zaidi ya 200 kutoka nchi mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ,
Mwenyekiti wa Kampuni ya Agricultural Non State Actors Forum (ANSAF),
Audax Rukonge, alisema serikali imekusudia kuweka kipaumbele kwenye
viwanda vya uchakataji wa mazao ya kilimo.
Kongamano hilo litalenga kuongeza uelewa miongoni mwa watunga sera
kuhusu mchango wa kilimo katika kuhamasisha ukuaji wa viwanda Tanzani.
“Wadau watajadili kupata tafsiri halisi ya sekta ya uchakataji mazao
ya kilimo katika muktadha wa mageuzi ya viwanda Tanzania,”alisema
Rukonge alisema kongamano hilo limedhaminiwa na USAID, Benki ya
Dunia,ANSAF,JICA na wadau wengine ambao wamesaidia kuleta watalamu
wakiwamo wakulima, watafiti,wafanyabiashara na watunga sera.
Mratibu wa Jukwaa la Sera ya Kilimo na Mchumi mwandamizi Wizara ya
Kilimo, Sophia Mlote alisema kongamano hilo la tatu litajadili maendeleo
ya kilimo nchini ikiwamo kujadili namna ya kutetea sera,sheria,kanuni.
Pia alisema kongamano hilo litajikita katika kujadili juu ya mpango
wa kilimo cha mihogo,mikunde, samaki, mazao, usafirishaji pamoja na
vifungashio kwa kuwa wazalishaji wengi hawana vifungashio.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269