Breaking News

Your Ad Spot

Jan 18, 2010

KIRUKACHO HUTUA! Jumbe arejea tena Msondo Band

         Mzee wa Dodo atua tena Msondo

                                                     Na Mdau wa Chachandu Daily
MWANAMUZIKI mwenye sauti yenye hadhi katika anga la muziki wa dansi hapa nchini, Hussein Jumbe, maarufu kama 'Mzee wa Dodo' hatimaye amerejea tena katika bendi ya Msondo.

Aliondoka nje ya bendi hiyo mwaka juzi, baada ya kuipua kibao cha  'Ajali' ambacho alikiimba kwa umahiri mkubwa akiwa na konvoy la bendi hiyo na marehemu TX Moshi William

Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye ni msemaji wa  Msondo amesema leo kwamba Msondo  wameamua kumrudisha kundini mwimbaji huyo baada ya  uongozi kukubaliana naye na sasa ameshaanza kupanda katika jukwani.

"Mpaka sasa tunajipanga kutoa nyimbo mpya za mwaka huu baada ya mwaka jana kutambulisha albamu yetu ya huna shukrani na kuwa ipo mtaani kwa sasa inauzwa" alisema Super D.
Bendi hiyo kwa sasa imekuwa ikitoa burudani za wazi katika kuwaweka karibu wapenzi wake ambapo kila jumamosi wanakuwa katika viwanja vya TCC Chan'gombe na Jumapili  Leaders Club jijini Dar es Salaam

2 comments:

  1. Anthony Angasiye Kisondella4/13/10, 9:14 AM

    Aha huyu Jumbe ni mpita njia tu, namuheshimu kwa tungo na uimbaji wake lakini tangu alipoingiwa na mdudu wa kuama bendi,inaoneakana tiba yake ni ngumu, Jumbe aliibuliwa na kuipaishwa kipaji chake pale alipochukuliwa na DDC Mlimani Park akitokea Urafiki Jazz miaka ile ya 1985. Nyota yake ilinga'a vilivyo huku akisaidiwa na wanamuziki kama Fransis Lubua (Marehemu), Mohamed Mwinyikondo (Marehemu), Adamu Bakari (Marehemu), Benno Villa Anthony, Shabaan Dede, Hassan Bitchuka, Hassan Kunyata, Abdallah Hemba. Ugonjwa ulianza pale alipokwenda Nairobi, aliporudi alipokelewa Sikinde, akutulia akaruka TOT, akutulia akaruka Msondo, akutulia akaruka Sikinde, akutulia akaruka Mikumi Sound, akutulia akaruka Sikinde, akutulia akaruka Msondo, Mara nikasikia ameanzisha bendi yake Talent Band, napo ajatulia ameruka Msondo. Nani wasi wasi sijui kama AMETUA nahisi kama bado MRUKAJI TU. Anyway kama ametua basi tunamuombea mema siye wadau wa muziki wa dansi wa enzi zileeeeeeeee!!

    ReplyDelete
  2. Anthony Angasisye Kisondella4/13/10, 9:34 AM

    Shukurani Bwana Bashir Nkoromo kwa hii post:

    Kwa mtizamo wangu namuona Hussein Jumbe kama mpita njia tu, namuheshimu kwa tungo na uimbaji wake lakini tangu alipoingiwa na mdudu wa kuama bendi,inaoneakana tiba yake ni ngumu, Jumbe aliibuliwa na kuipaishwa kipaji chake pale alipochukuliwa na DDC Mlimani Park akitokea Urafiki Jazz miaka ile ya 1985. Nyota yake ilinga'a vilivyo huku akisaidiwa na wanamuziki kama Fransis Lubua (Marehemu), Mohamed Mwinyikondo (Marehemu), Adamu Bakari (Marehemu), Benno Villa Anthony, Shabaan Dede, Hassan Bitchuka, Hassan Kunyata, Abdallah Hemba. Ugonjwa ulianza pale alipokwenda Nairobi, aliporudi alipokelewa Sikinde, akutulia akaruka TOT, akutulia akaruka Msondo, akutulia akaruka Sikinde, akutulia akaruka Mikumi Sound, akutulia akaruka Sikinde, akutulia akaruka Msondo, Mara nikasikia ameanzisha bendi yake Talent Band, napo ajatulia ameruka Msondo. Nani wasi wasi sijui kama AMETUA nahisi kama bado MRUKAJI TU. Anyway kama ametua basi tunamuombea mema siye wadau wa muziki wa dansi wa enzi zileeeeeeeee!!

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages