Breaking News

Your Ad Spot

Jan 15, 2010

KAMPENI KAMAMBE DHIDI YA MALARIA WAZINDULIWA DAR





WAZIRI wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa (katikati) akisikiliza hotuba ya aliyekuwa Balozi Marekani nchini, Mark Green (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza Maralia kwenye Hoteli ya Movenpick leo. Kulia ni Bw. Peter Peter Chernin (Mwenekiti wa Malaria no More Marekani ) ambaye ameungana na Balozi Mark Green katika kampeni hiyo. Shoto ni Naibu waziri wa Afya Dk. Aisha Kigoda.

Rais akiwa na  mwanamuziki Baba Zorro katikauzinduzi huo

JK akiwa na Bi Kidude katikauzinduzi huo

JK akiwa na Jide kataika uzinduzi huo

JK akiwa na Marlow katika uzinduzi huo

JK akiwa na Profesa Jay katikauzinduzi huo

fULL STORy
WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imetangaza kuwa leo mheshimiwa Raisi Jakaya  Kikwete amekubali kuongoza kampeni ya "Malaria Haikubaliki: Tushirikiane Kuitokomeza".

Wizara hiyo imeungana na wasanii mashuhuri wa Tanzania, washirika wa kimataifa na viongozi wa serikali, wafanyabiashara na vitengo vya sanaa kulitangazia Taifa tamasha la zinduka hapo tarehe februari 13, mwaka huu katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam. Tamasha hili ni la kuwahamasisha watanzania katika kupambana na malaria.

Mwaka huu Tanzania itakuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufanikisha zoezi la utumiaji wa chandarua ya mbu na kutolewa kwa gharama nafuu kwa raia wake. Katika kuhamasisha juhudi hizi, Raisi kikwete na Malaria haikubaliki inahamasisha kila mtanzania kuwa na jukumu la kujilinda mwenyewe na familia yake katika kuidhibiti malaria.

Tanzania, kama kiongozi wa kupambana na malaria ulimwenguni, inahamasisha sekta zote za kijamii zikiwamo sekta za sanaa, biashara, na michezo kujumuika pamoja kupambana na malaria nchi nzima.

Chini ya uongozi wa Rais na wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kampeni hii ya uhamasishaji imelenga kila jamii ya kitanzania ili kubadili mtazamo wa watanzania juu gonjwa hili la malaria.

Matokeo ya juhudi hizi ni kuongeza ujuzi zaidi wa kujikinga na malaria kama kulala ndani ya chandarua kilichowekwa dawa, tambua na itibu malaria mapema na hakikisha unajali na kuangalia afya ya mama mjamzito.

Waafrika wengi hudhani malaria haiepukiki, na kwamba hakuna wanachoweza kufanya katika kuzuia gonjwa hili. Tunakwenda kuwahakikishia kuwa sio sahihi. Tunaweza kupunguza vifo vitokanavyo na malaria” alisema Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii David Mwakyusa.

Katika shughuli za mwaka 2010, Raisi Kikwete ataongoza tamasha la kitaifa liitwalo zinduka litakalowashirikisha wasanii mashuhuri wa Tanzania akiwamo msemaji mkuu wa tamasha hili lady Jay dee, Professor Jay, Tanzania House of Talent (THT na wengine wengi.

Kuipitiua vituo vya luninga na redio ujumbe wa tamasha hili utaweza kuwafikia mamilioni ya watanzani na ujumbe mahususi wa kutambua jukumu lao katika kujikinga na ugonjwa wa malaria.

Wasanii hao mahiri wa Tanzania wametunga wimbo wa pamoja unaozungumzia athari za ugonjwa wa malaria, wimbo uliowashirikisha wasanii 18. Wimbo huo umetambulishwa kwa waandishi wa habari na utaimbwa siku ya tamasha la zinduka.

"Ulimwengu wa muziki unanafasi kubwa katika kufikisha ujumbe kwa watanzania katika kupambana na malaria na kupata mafanikio makubwa katika kupambana na ugonjwa huu, alisema Lady Jay D kama msemaji wa wasanii walio katika kampeni hii. "Watanzania wote wataweza kupaza sauti zao kwa njia ya wimbo kwa nia moja ya kusitisha malaria nchini".

Shughuli kibao za ushirikiano za kijamii, ujumbe kwa njia ya luninga na radio,mabango,ngazi ya jamii,kiutamaduni, matukio ya kimichezo na maonyesho ya barabarani ili kuhakikisha ujumbe wa malaria haikubaliki unaufikia kila familia nchini Tanzania.

Kampeni hii ya kitaifa itakuwa kwenye engo zote za ngazi ya kijamii na kila nyumba kwa kuhamasisha shughuli za kijamii zitakazotolewa na Population Services International ,Johns Hopkins University na shughuli za district advocacy zitakazoongozwa kwa sauti moja. Wakati huo huo chama cha msalaba mwekundu Tanzania kitakuwa katika kampeni za nchi nzima.

Kampeni ya Malaria Haikubaliki pia imehusisha baraza la kiristo nchini na baraza la kiislam kuwahusisha viongozi wa kiimani na waumini wao kuweka juhudi katika kupambana na malaria nchi nzima.

Barani Africa malaria haiathiri maisha ya watu tu bali jamii nzima. Husababisha mtu mmoja kukosa kazini kwa siku kumi na tano ndani ya mwaka familia inatumia zaidi asilimia 25 ya kipato cha familia katika kutibu malaria barani Africa.

Malaria ni kikwazo katika maendeleo, inakadiriwa barani Afrika dola bilioni 12 kila mwaka zinapotea na asilimia 40 zinatumika katika masuala ya afya.katika kupambana na ugonjwa huu, Tanzania imeweza kuonyesha jinsi Africa peke yake inavyoweza kujikwamua kutoka kwenye mzigo wa malaria na kuendeleza mikakati yake ndani na nje ya mipaka.

Malaria Haikubaliki: Tushirikiane Kuitokomeza inaongozwa na serikali ya Tanzania na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Washirika wengine katika kampeni hii ya kupinga malaria ni Roll Back Malaria Partnership, Malaria No More, Population Services International, Johns Hopkins University Center for Communication Programs, Tanzanian Red Cross, United Against Malaria, MEDA na World Vision with support from the Global Fund.

Ciao

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages