Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akisalimia wananchi wakati Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (aliyeshika kinasa sauti), alipokagua jana mradi wa ujenzi wa daraja la mto Muntapu, linaloendelea kujengwa kwa nduvu za Halmashauri ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvumaikishirikiana na nguvu za wananchi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (aliyenyoosha mkono) akikagua ujenzi wa daraja la Lukumbo-Mchoteka, linalojengwa katika mto Muntapu, Tunduru mkoani Ruvuma jana. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenbezi Nape Nnauye.
Ndugu Kinana na Dk. Asha-Rose Migiro wakitupa udopngo kwa sepetu wakati wakishiriki ujenzi wa daraja la Lukumbo-Mchoteka, wilayani Tunduru. Kushoto ni Nape akisubiri kumpokea sepetu Dk. Asha-Rose
"NAAM MRADI HUU NI UTEKELEZAJI MZURI WA ILANI YA CCM" Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimweleza Nape wakati wakikagua ujenzi wa daraja hilo
Kinana na Dk. Asha-Rose Migiro wakiondoka kwenye daraja hilo linalojengwa
ILIKUWA SIKU YA ASIYE NA MWANA ABEBE JIWE: Wakazi wa Mchoteka Kata ya Machoteka, wilayani Tunduri mkoani Ruvuma, wakimsubiri kwa hamu katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alipokwenda kukagua ujenzi wa nyumba ya mwalimu katika shuke ya sekondari ya Kata hiyo, jana
Hapa Dk. Asha-Rose Migiro, Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa hakimbizi Mwenge wa Uhuru, bali alikuwa ameshika tawi lake la mti wakati wa mchakamchaka uliongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kwenda kukagua ujenzi wa shule ya sekondari ya Kata ya Machoteka, wilayani Tunduru jana.
Waandishi wa habari walioko katika msafara wa ziara ya Kinana mkoani Ruvuma, wakiwa katika hekaheka za kutafuta matukio mbalimbali, msafara huo ulipofika kata ya Mchoteka, Tunduru jana
Hapa kazi tu: Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akitupa udongo kutoka shimoni wakati aliposhiriki kuchimba mtaro kwa ajili ya ujezi wa maabara kwenye shule ya sekondari ya Mchoteka, wilayani Tunduru mkoani RuvumaKatibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisaidia kuweka dirisha kwenye chumba cha jengo la nyumba ya mwalimu alipokagua ujenzi wa nyumba hiyo kwenye shule ya Mchoteka, wilayani Tunduru mkoani Ruvuma
Mamia ya wananchi wakiwa wamefurika katika mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alipowasili katika kijiji cha Nalasi, wilayani Tunduru mkoani Ruvuma jana
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza kwa hisia kali, alipohutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana, katika kijiji cha Mtina, wilayani Tunduru mkoani Ruvuma
"HAKIKA HIKI NDICHO CHAMA" Baadhi ya wazee katika kata ya Nalasi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM, Abdyulrahman Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye kata hiyo, wilayani Tunduru mkoani Ruvuma, jana
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269