Breaking News

Your Ad Spot

Jun 19, 2014

Airtel Divas watoa msaada kwa wanawake wasiojiweza

 Mgeni Rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kazi Services Ltd, Zuhura Muro (kushoto), huku akisaidiwa na Makamu Mwenyekiti wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’, Happy John wakikata keki kuashiria uzinduzi rasmi wa kikundi hicho, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika uzinduzi huo, Airtel iliweza kukisadia Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA), kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba). Wanaoshuhudia ni wanachama wa Airtel Divas. 
 Mgeni Rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kazi Services Ltd, Zuhura Muro (wa pili kulia), akiangalia moja ya bidhaa zilizotengenezwa na Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA ) cha Kinondoni, kabla ya kuzindua rasmi Kikundi cha wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’,  katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika uzinduzi huo, Airtel iliweza kuisadia SWAUTA, kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba). Kushoto ni mwanachama wa Swauta, Adelina Mluge.
  Wanachama wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’, wakichagua bidhaa zilizotengenezwa na kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Airtel Divas, uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika uzinduzi huo, Airtel iliweza kuisadia SWAUTA, kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba). 
 Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kazi Services Ltd, Zuhura Muro (kushoto), akijadiliana jambo na Afisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde (kulia), baada ya kutembelea bidhaa zilizotengenezwa na Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, kabla ya kuzindua rasmi Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’,  katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika uzinduzi huo, Airtel iliweza kuisadia SWAUTA, kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).
 Wanachama wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’, wakilisakata rhumba, katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kikundi hicho, uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika uzinduzi huo, Airtel iliweza kukisadia Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba). 
 Mgeni Rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Kazi Services Ltd, Zuhura Muro, akifurahia zawadi ya kitenge baada ya kukabidhiwa zawadi na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Adriana Liamba (kulia), katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’, iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika uzinduzi huo, Airtel iliweza kukisadia Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, kuuza bidhaa zao kwa bei ya juu na kupata pesa kwa ajili kulipia banda lao lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).
Picha ya Pamoja

========  ========
Umoja wa wafanyakazi wanawake wa Airtel ujulikanao kama Airtel Divas umejitoa kuwasaidia na Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA )  kilichopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Wafanyakazi hao wa Airtel walifanya uzinduzi rasmi wa Airtel Divas  na kualika kikundi cha SWAUTA kuonyesha na kuuza bidhaa zao kwa wafanyakazi wa Airtel na kuwawezesha kupata fedha kwaajili ya kuwa na banda lao katika maonyesho ya 38 ya kimataifa  ya SABASABA.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo Meneja Rasilimali watu Sophia Melamali alisema” tunayofuraha kuzindua rasmi Airtel Divas mpango maalumu wenye lengo la kuwainua na kuwahamasisha wanawake na wafanyakazi wa Airtel kuzifikia ndoto zao. Kama tunavyofahamu wanawake wanayo majukumu makubwa ya familia na kazi,  hivyo kuwa na changamoto kubwa ya kugawa muda wao kwa ufanisi. kwa kupitia Airtel Divas tunashirikiana kwa pamoja kupeana ujuzi na mawazo ya namna ya kupambana na changamoto hizi na kufikia mafanikio katika malengo tuliyojiwekea.

Sambamba na hilo tunawahamasisha wanawake kushiriki katika kujitolea na kutoa msaada kwa jamii na ndo maana leo tumewaalika kina mama hawa wenye ulemavu na kuwapa nafasi ya kuuza bidhaa zao na kiasi cha pesa watakachopata leo tutakiongeza mara mbili na kuwawezesha kupata fedha za kutosha kulipia banda katika maonyesho ya sabasaba. Tunaamini kwa kufanya hivi tutawawezesha kukuza biashara yao. Natoa wito kwa watanzania watakaopata nafasi ya kwenda kwenye maonyesho haya wapate nafasi ya kuwatembelea na kuwaaunga mkono pia.

Akiongea mara baada ya kukabithia msaada huo mwenyekiti Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania SWAUTA bi Stella Jairosi Alisema, Tunawashukuru Airtel kwa kutuwezesha kupata banda zuri liliopo eneo zuri katika maonyesho ya Sabsaba, kwa miaka 8 sasa tumekuwa tukishiriki katika maonyesho haya lakini hatukuwahi kuwa na banda letu wenyewe. Kupitia msaada huu kutoka Airtel kutatupatia mwanya wa kuonyesha bidhaa zetu na kupata mwaya wa kuuza kwa soko la ndani na la nje na pia kutatusaidia kuuza bidhaa zetu kwa kiasi kikubwa na kuongeza pato letu na hivyo kuendeleza miradi ambayo hatukuweza kuifanya kutokana na uhaba wa fedha.

Kwa upande wake mgeni rasmi na Mkurugenzi Mkuu wa Kazi Services Ltd, Zuhura Muro alisema“ nimejisikia furaha kuwa mgeni rasmi katika shughuli ya leo na napenda kuwapongeza sana Airtel Divas kwa kujitolea kusaidia jamii kupitia shughuli hizi za huduma kwa jamii wakiwemo wa mama hawa wa kikundi cha walemavu nawahamasisha muendelee na juhudi hizi.Pamoja na hayo pia nachukua nafais hii kuwahimisha Airtel Divas kufanya kazi kwa bidii na kuonyesha uwezo wao katika maeneo yao ya kazi ili waweze kupata nafasi nyeti katika Uongozi

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages