Mwenyekiti
na mwasisi wa kikundi cha kujitolea kinachowalea watoto wenye mfanano
wa kikundi cha Trabajo Voluntario, Marisa Yussuf Himid akionyesha bango
wakati maandalizi ya shughuli hiyo.
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
ZAIDI
ya watoto mfanano 50 na familia zao wanatarajiwa kujumuika na watu
wengine katika viwanja vya Ngome Kongwe kwa mashamushamu ya kuonesha
upendo na kushuhudia mateso yanayowapata watoto hao.
Taasisi
isiyo ya kiserikali ya kujitolea ya mjini Zanzibar ya Trabajo
Voluntario, (Voluntary Work) inakutanisha watoto hao wakishirikiana na
taasisi isiyo ya kiserikali ya tamasha la filamu la kimataifa la
Zanzibar (ZIFF).
Kwa
mujibu wa mmoja wa maofisa wa Trabajo Voluntario, Marissa Himid Yusuf
taasisi hiyo iliyoanzishwa mwaka 2005 ili kusaidia watoto mfanano,
lengo lao kubwa la kuwakusanya hapo ni kuwaonesha upendo na pia kujadili
maslahi yao.
Alisema
kwa sasa watoto wengi wenye hali ya ufanano hawatimiziwi haki zao
msingi ikiwemo ulinzi na wala hakuna sera inayohakikisha kwamba
wanalindwa na wanapewa haki nyingine kama watoto wengine hasa elimu
itakayowawezesha kuwa na kitu cha kufanya katika maihs ayao.
Alisema
katika maelezo yake kwamba kuna simulizi za kutisha kuhusu watoto hao
na kwamba wapo baadhi ya wanwake wapo tayari kutoa nushuhuda wa
yaliyotokea katika famulia zao baada ya watoto walionao kubainika kwamba
wana tatizo la mfanano.
Alisema
pamoja na ushuhuda huo mkusanyiko huo umelenga pia kukemea maovu
wanayofanyiwa watoto hao na watu wazima kwamkusanyiko huo ni
kuelimishana kuhusu watoto hao na kuhimiza ushiriki wa serikali na jamii
kuhakikisha usalama wao na kupata haki yao ya msingi ya kupendwa na
kulindwa.
Alisema
pamoja na kuwapo kwa haja ya sera zinazotekelezeka ili kutoa ulinzi kwa
watoto na familia zao, ipo haja kw ajumuia kuondoa unyanyapaa dhidi
yao. Kwa kusanyiko hilo la Ijumaa tunategemea
wananchi watakuja kujifunza kuondokana na unyanyapaa na pia kufanya
kampeni ya kuondoa hali hiyo miongoni mwa jamii.
Marisa
Yussuf Himid, ambaye pia ni mwanzilishi na Mkurugenzi wa taasisi hiyo
ya TrabajoVoluntario, alisema mamlaka zinaozhusika zinaonekana kukimbia
jukumu la kulea watoto hao ambao wana manufaa makubwa katika jamii
wakielekezwa na kujua.
Aidha
alitumia wasaa kuiomba serikali na mamlaka zake kuangalia suala la
kunyan yaswa kwa watoto hawa, kufuatilia na kuwafikisha kizimbani wale
wote wanaowatesa watoto hao kwa namna mbalimbali ikiwemo kuwabaka,
kuwanajisi na hata kuwalawiti. Aidha ametaka shule kutumika kufunza watoto hawa ambao elimu yao huchukua muda mrefu.
Kwa mujibu wa Marissa mgeni rasmi atakuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya ulemevu, AbedaAbdallah Rashid, ambaye atazungumza.
Aidha balozi wa watoto mfanano Fareed Kubanda, atazungumza wakati wa kufunga kusanyiko hilo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269