Na. Richard Bakana-shaffihdauda.com
Klabu
bingwa barani Ulaya usiku huu imeendele kwa mchezo mmoja kati ya
Juventus kutoka Italia pamoja na Real Madrid ya Spain ambapo Muargentina
ambaye aliachwa katika fainali za kombe la Dunia 2014 nchini Brazil,
Carlos Tevez akiihakikishia timu yake ushindi wa Bao 2-1.
Katika
mchezo huo Juventus ndio walianza kupata bao katika dakika ya 8 kupitia
kwa Morata bao ambalo halikudumu sana kwani kunako dakika ya 27 Mreno
Cristiano Ronaldo akasawazisha bao akiunganisha krosi safi ya James
Rodriguez nakufanya timu hizo zinaenda kupumzika zikiwa 1-1.(P.T)
Baada ya kipindi cha pili kuanza Tevez ambaye kwasasa anafanya vyema kwa kucheka na nyavu, katika dakika ya 57 akaiandikia Juventus bao la pili na la ushindi kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United pamoja na Manchester City kufanyiwa madhambi na kuangushwa ndani ya 18 na beki wa Real Madrid Carvajal.
Vikosi vya timu zote mbili vilikuwa kama ifuatavyo.
Juventus: Buffon, Lichtsteiner, Bonucci, Chiellini, Evra, Marchisio, Pirlo, Sturaro, Vidal, Tevez, Morata
Subs: Storari, Barzagli, Padoin, Pepe, Pereyra, Llorente, Matri.
Real Madrid: Casillas, Carvajal, Varane, Pepe, Marcelo, Ramos, Kroos, Rodriguez, Isco, Bale, Ronaldo.Subs: Keylor Navas, Coentrao, Hernandez, Lucas Silva, Arbeloa, Jese Rodriguez, Illarramendi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269