Breaking News

Your Ad Spot

Feb 21, 2016


Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa BAWACHA na Mbunge Viti Maalumu Taifa Grace Tendega (katikati) jana February 20,2016 akizindua ofisi Mpya ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Chadema, Susan Masele (Kulia). Kushoto ni Paschazia Renatus ambae ni Katibu wa Bawacha Mkoa wa Mwanza.

Akizungumza katika Uzinduzi huo, Tendega alipongeza uwepo wa ofisi hiyo ambayo itakuwa ikisikiliza kero za wananchi bila kujalisha itikadi zao za kisiasa kwa ajili ya kupokea hoja za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi ikiwemo kuzisemea bungeni.

"...Kazi ya Mbunge siyo kugawa hela. Kazi ya Mbunge ni kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua. Na mimi niseme nitakuwa mwakilishi bora na hapa tumeanza tu ambapo katika ofisi hii nitakuwa napokea na kusikiliza kero za wananchi na kwenda kuzisemea bungeni... Alisema Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Chadema, Susan Masele.
Ofisi hiyo inapatikana Mtaa wa Ghana Green View, Kata ya Nyamanoro, Jimbo la Ilemela Mkoani Mwanza. Ndani yake pia kuna Ofisi ya BAWACHA Mkoa wa Mwanza.
Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa BAWACHA na Mbunge Viti Maalumu Taifa Grace Tendega (katikati) jana February 20,2016 akizindua ofisi Mpya ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Chadema, Susan Masele. Kushoto ni Paschazia Renatus ambae ni Katibu wa Bawacha Mkoa wa Mwanza.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages