Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
limeanzisha mazoezi makubwa yanayojumuisha ndege aina mbali mbali za
kivita katika eneo la Anarak, Isfahan, kati mwa Iran.
Kwa mujibu wa Kanali Masoud
Ruzkhush, msemaji wa Mazoezi ya Sita ya Nguvu za Anga za Waliojitolea
Kulinda Anga ya Wilayat, luteka hiyo itaendelea kwa muda wa siku
tatu kuanzia leo Jumapili na kushirikisha ndege mbali mbali za kivita.
Aidha amesema ndege za kukusanya habari
za kijasusi na pia ndege maalumu za kujaza mafuta ya ndege nyingine za
kivita zikiwa angani pia zinashiriki katika mazoezi hayo. Halikadhalika
amebaini kuwa, katika mazoezo hayo ni sehemu ndogo tu ya uwezo wa jeshi
la anga la Iran utakaoonyeshwa.
Ndege zinazoshiriki zitafanya mazoezi
kuhusu kuweka mafuta katika ndege ya kivita ikiwa inaruka ingani
inaruka, umahiri wa kulenga shabaha hasa nyakati za kiza totoro
cha usiku na pia kufanyia majaribio maroketi ya anga kwa anga na anga
kwa ardhi n.k.
Kati ya ndege za kivita zinazoshiriki
katika mazoezi hayo ni Sa’eqeh iliyotengenezwa hapa Iran na pia F-14,
Sukhoi Su-24, and MiG-29.
Iran hufanya mazoezi makubwa ya kijeshi
mara kwa mara ili kubaini uwezo na utayarifu wa vikosi vya ulinzi wa
kuihami nchi. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasisitiza kuwa, uwezo wake
wa kijeshi si tishio kwa nchi yoyote bali sera zake za ulinzi
zimejengeka katika msingi wa kujihami na kukabiliana na adui.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269