Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (kulia) akiungana
kuimba wimbo wa Taifa na Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya
Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) Mhe. Waziri
wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.
Angellah Kairuki (kushoto) na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na
Utawala Bora, Bahame Nyanduga, kwenye ufunguzi wa maadhimisho hayo
liliyofanyika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (kulia) akieleza
uzoefu wake kuhusu shughuli za Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) kwenye
kongamano hilo.
Baadhi ya
viongozi wa Serikali waliohudhuria Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka
50 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) kwenye ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es Salaam wakiongozwa na Rais Mstafu wa Awamu ya
Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa pili kulia) wakifuatalia taarifa ya
Jaji Mst. Lubuva.Wengine ni Mawaziri Wakuu Wastaafu Fredrick Sumaye
(kulia), Jaji Mstaafu Joseph Warioba (wa tatu), na Mwanasheria Mkuu
Mstaafu Jaji Mack Bomani na Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora Jaji Kiongozi Mstaafu Amiri Manento.
Baadhi ya
Wageni Waalikwa wakiwemo kutoa Ubalozi wa Sweden nchini Tanzania na
Wawakilishi wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi za nchi za Afrika,
wakifuatilia taarifa ya Jaji Mst. Lubuva.
Rais
Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhaj Ali
Hassan Mwinyi akipokea tuzo ya Heshima ya Utawala Bora kutoka kwa Mgeni
Rasmi wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa Tume ya
Kudumu ya Uchunguzi (TKU) Mhe. Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki kwenye ukumbi wa
Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (katikati) akiwa
amepokea Cheti cha Utambuzi wa Utumishi wake kwenye Tume ya Kudumu ya
Uchunguzi (TKU) kutambua mchango wake.Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Bahame Tom Nyanduga na kulia
ni Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Mary Massay.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (wa tatu kulia)
akiungana na kwenye picha ya pamoja na na Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya
Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi
(TKU) Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj
Ali Hassan Mwinyi na Viongozi wengine wa Serikali Wastaafu waliohudhuria
maadhimisho hayo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam..
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva, akisalimiana na
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva akimueleza jambo
Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa
Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki baada ya
ufunguzi wa maadhimisho hayo.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva, akibadilisha
mawazo na Wanasheria Wakuu wa Serikali Wastaafu wenzanke Jaji Mst. Mark
Bomani 1965-1976 na Jaji Mst. Joseph Sinde Warioba 1976 -1985.Jaji Mst.
Warioba alitumikia nafasi hiyo kuanzia mwaka 1985 hadi 1993.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva akizungumza na
kituo cha Televisheni cha ITV baada ya ufunguzi wa Maadhimisho ya
Kumbukumbu ya Miaka 50 ya Kuanzishwa kwa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi
(TKU) Picha na Hussein Makame-NEC
Hussein Makame, NEC
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva ameitaka Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kujifunza uzoefu wa tendaji wa
Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) ili kuimarisha utawala bora nchini.
Jaji Mst.
Lubuva ametoa wito huo wakati akeleza uzoefu wake juu ya utendaji kazi
wa Tume ya Kudumu ya Uchunguzi (TKU) wakati wa Maadhimisho ya Miaka 50
ya Tume hiyo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es
Salaam.
Alisema
pamoja na TKU kukabiliwa na changamoto nyingi katika inatekeleza
majukumu yake wakati huo lakini ilifanya kazi zake kwa ufanisi kutokana
na malalamiko ya wananchi yaliyoshughulikiwa kwa wakati huo.
“Katika
hali na mazingira ya Tume ya wakati huo, bila kusita nashawishika kusema
kuwa Tume ya Kudumu ilianzishwa wakati ambapo si watu wengi kwa bahati
mbaya Afrka ambao walijali haki za binadamu na utawala bora” alisema
Jaji Mst. Lubuva.
Aliongeza
kuwa itakuwa si kusifia kusema kuwa TKU ilifanya kazi nzuri katika
kipindi chake cha miaka 32 kwani ulikuwa wakati ambapo Tanzania ndio
ilikuwa imejikomboa kutoka utawala wa Kikoloni na ilijitahidi kuendesha
shughuli za maendeleo kwa wananchi.
Hata
hivyo alisisitiza kuwa walithubutu kwa mwalimu kuleta wazo la kuanzisha
TKU ili kunusuru wananchi kutakona na madhila ya matumizi mabaya ya
madaraka ya viongozi na watendaji kwa wakati huo.
“Kwa
upande mwingine Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ina kibarua
kizito katika kutekeleza majukumu yake katika mazingira ya sasa ambapo
tume hii si rahisi kuelezea kwa wananchi kwa nini isifanikiwe zaidi ya
TKU”
Alisema
THBUB tofauti na TKU ina bahati ya kujifunza kutokana na uzoefu wa tume
hiyo ya kudumu katika mazingira ya sasa kulinganisha maendeleo na uelewa
wawananchi kiujumla kuhusu haki zao za kimsingi kisiasa na kiutawala.
“Hivyo
tunaposherehekea miaka 50 ya Tume ya Uchunguzi ni halali kusema kwamba
ilikidhi haja na matakwa ya wananchi kwa wakati huo kuweka misingi imara
ambayo THBUB itaitumia katika juhudi za kusonga mbele”alisema Jaji Mst.
Lubuva.
Kwa
upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejiment ya Utuishi wa Umma
Mhe. Angellah Kairuki alisema lengo kubwa la Serikali kuanzisha TKU
ilikuwa ni kumlinda mwananchi na lilifanikiwa kwa kushughulikia
malalamiko 39,000 kwa kipindi cha miaka 35.
“Aidha
malalamiko yaliyopokelewa katika kipindi cha miaka 15 (2001-2016) ya
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ni 32,000 na hivyo kufanya
idadi ya malalamiko ya miaka 50 kufikia 71,000” alisema Mhe. Waziri
Kairuki na kuongeza kuwa:
“Idadi
hiyo inaonesha jinsi vyombo hivi vilivyo na manufaa kwa wananchi
wanyonge.Baadhi ya malalamiko yaliyopokelewa ni kuhusu vitendo vya
unyanyasaji, masuala ya utumishi, kuchelewa kutekeleza wajibu, ,
kukataliwa kuomba rufaa, kutrofuata taratibu za kisheria, mirathi,
matumizi mabaya ya mali ya umma na migogoro ya ardhi”
Naye
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bahame Nyanduga
alisema Maadhimisho ya Miaka 50 ya TKU yamekwenda sanjari na kumuenzi
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kwa kuanzisha Tume hiyo ikiwa ni
taasisi ya kusimamia uwajibikaji wa watumishi wa umma kwa wananchi.
“Pili ni
kujikumbusha huko tulikotoka na kujifunza kutokana na kazi za TKU,
changamoto na na mafanikio iliyoyapata na mwelekeo unaotakiwa katika
kuhakikisha dhana ya uwajibikaji na utawala bora zinaendelezwa nchini
Tanzania” alisema Nyanduga.
Katika
maadhimisho hayo Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Rais Mstaafu Ali
Hassan Mwinyi walipata Tuzo na Cheti cha kutambua mchango wao kuweka
misingi ya uwajibika na utawala Bora. (P.T)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269