.

MFALME MOHAMMED VI WA MOROCCO AWASILI JIJINI DAR ES SALAAM

Oct 23, 2016

01

Mfalme  Mohammed VI wa Morocco akishuka kwenye ndege iliyomleta akiwa ameongozana na ujumbe wake mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere  International Airport (JNIA) jijini Dar es salaam  leo Oktoba 23, 2016

Mfalme huyo amepokelewa  na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli jioni hii, Mfalme Mohammed VI atakuwa nchini kwa ziara rasmi ya siku tatu.

(PICHA NA JOHN BUKUKU WA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)

02
Mfalme  Mohammed VI wa Morocco akipokea shada la maua mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa JNIA leo jioni.

001
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli akisalimiana na mgeni wake Mfalme Mohammed VI wa Morocco mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa JNIA jijini Dar es salaam jioni hii.

1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli akielekea karibu na ndege iliyomleta mgeni wake Mfalme Mohammed VI wa Morocco mara baada ya kuwasili jijini Dar es salaam.

2 3
Mfalme Mohammed VI wa Morocco akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange akiwa ameongozana na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli.

4
Mfalme Mohammed VI wa Morocco akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Ernest Mangu huku  akiwa ameongozana na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli.

5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli akimtambulisha Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa Dk. Modestus Kipilimba kwa Mfalme Mohammed VI wa Morocco wakati alipowasili jijini Dar es salaam leo.

6
Mfalme Mohammed VI wa Morocco akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Magereza Kamishna John Casmir Minja huku  akiwa ameongozana na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli.

7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli akiongozana na Mwenyeji wake Mfalme Mohammed VI wa Morocco mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa JNIAleo jioni.

9
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mgeni wake Mfalme Mohammed  VI wa Morocco.

11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli akiangalia vikundi vya ngoma na  Mgeni wake Mfalme Mohammed  VI wa Morocco wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa JNIA jijini Dar es salaam.

12
Mfalme Mohammed  VI wa Morocco akipungia mkono wananchi waliojitokeza kumlaki huku akiwa na Mwenyeji wake  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli.

13
Ndege iliyomleta Mfalme Mohammed  VI wa Morocco ikiwasili.

14
Ndege iliyomleta Mfalme Mohammed  VI wa Morocco ikijiandaa kutua kwenye uwanja wa Ndege wa JNIA.

15
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumlaki Mfalme Mohammed  VI wa Morocco wakati alipowasili jijini Dar es salaam . 

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª