NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA
MWANAMKE mmoja Ester Mwambene
anayekadiriwa kuwa na miaka (50) mkazi wa mbeya amenusurika kupigwa na wananchi
wa Mtaa wa Mlole Halmashauri ya Kigoma Ujiji wilaya ya kigoma Mjini, baada ya
kuhusishwa na jaribio la mauwaji kwa njia ya nguvu za giza.
Tukio hilo lilijiri saa 2,00
usiku wa 16,0ctoba,2016 wakati Penina
akila chakula cha usiku na mdogo wake nje ya kibaraza chao ghafla alitokea bi
mkubwa huyo akiwa ameketi kitini na kumuliza maswali kadhaa kwa dakika tano na
alipoanza kuondoka ndipo binti akanguka chini.
Akizungumza na Jamboleo mdogo wa
binti huyo Sada Said alisema mama yake penina alimkamata bi mkubwa huyo na
kumuliza kulikoni na majirani wakasogea katika tukio wananchi walitaka kupiga
mwanamke huyo lakini kwa hekima za mchungaji aliyetambuliwa kwa jina la Meshack
alitoa neno la mungu kwa mwanamke aliyeshukiwa kuwa ni mchawi.
Alifafanua kuwa wakati mchungaji
huyo akimwombea mwanamke huyo ghafla Penina alianza kutapika damu na uchafu wa
madawa katika kinywa chake ndipo raia walianza kumpekua mshukiwa na kumkuta na
mchanga,madawa katika moja ya nguo alizovaa hatimaye walizipoka na kuzichoma
moto.
Said akiri baada ya maombi mazito
nduguye alikuwa akiongea maneno yasiyoeleweka huku mwanamke huyo akidai
alitumwa na wachawi wenzake kutoka sumbawanga amchukue binti huyo bila kutoa
sababu za msingi na walipomdadisi sana alipoteza mada.
Alipohojiwa Mwenyekiti wa Mtaa
huo Diye Paulo akiri kumpokea mwanamke
huyo saa 6.00 za usiku nyumbani kwake na amegundua akiri yake ina shida na kuwakabidhi mgambo wakae nae katika genge
kubwa la Mkatutu ambalo wanalinda lakini hajui kama alifanya jaribio hilo.
Paulo alifafanua kuwa,mwanamke huyo
alitoa maelezo yanayochanganya lakini leo (jana)amezungumza kwa njia ya simu na
kijana wake aliyemtaja kuwa ni Tumaini Kazembe ambaye ni mtoto wa mwanamke huyo kwa mujibu
wake na amekiri kumtumia fedha mwenyekiti huyo ili amsafirishe mkoani
sumbawanga.
Gazeti hili lilipojaribu kuzungumza
na mshukiwa wa tukio hilo Mwambene alisema mwane amelazwa maweni mwanae
amevunjika mguu na alipoulizwa ni mkazi wa wapi alidai anaishi kigoma kijiji
cha kalinzi wilaya ya kigoma vijijini.
Gazeti hili lilipewa namba za
simu za mmoja wa jamaa wa mwanamke huyo Nathaniel Luka alisema mwanamke huyo
ana tatizo la akiri kwani kwa muda amekuwa akipotea katika mikoa ya
sumbawanga,mpanda na kigoma kila anapokwenda anatabia ya kupotea na kukiri kumfuatilia ili wamrudishe mbeya.
Alipoulizwa Kamanda wa Polisi
Ferdinand Mtui kuhusu hilo alisema hajui na kuahidi kulifuatilia suala hilo
kupitia wakuu wa vitengo husika.mwisho.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269