Na Magreth Magosso,Kigoma
MKUU wa Wilaya ya Kibondo Kanali Hosea
Ndagala ameitaka Kamati ya ushauri wa
watumiaji wa usafiri wa Nchi kavu na Majini(SUMATRA) Mkoa wa Kigoma isimamie kwa umakini haki za
watumiaji wa usafiri wa vyombo vya moto sambamba na utoaji wa leseni kwa
madereva wa usafiri husika.
Kanali Ndagala aliyasema hayo
mwishoni mwa wiki katika kongamano la Klabu
za wanafunzi wanaotoa elimu ya usalama barabarani na haki za mtumiaji wa
usafiri wa nchi kavu na majin( SUMATRA)uliofanyika kigoma ujiji ,uliolenga kuwakumbusha
wajibu wao kwa jamii namna ya kulinda
maslai yao hasa umuhimu wa utunzaji wa tiketi pindi ajali itokeapo.
“nipo hapa kwa niaba ya mgeni
rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa,endeleeni kusimamia haki za watumiaji kwa
kuthibiti utoaji wa leseni kwa watu wasio na sifa za kupewa leseni,na abiria katika
usafiri wa aina yeyote adai tiketi itamsaidia katika kudai haki pindi ajali
inapotokea” alisisitiza Mkuu wa wilaya hiyo.
Akisoma risala ya utendaji kazi
wa kamati hiyo Mwenyekiti Flora Fundi alisema klabu za wanafunzi ni chachu ya
jamii kutambua serikali inajali usalama wa maisha yao katika utumiaji wa
usafiri,ambapo kupitia kamati wamefanikiwa kutatua kero na kusimamia malalamiko mbalimbali ya watumiaji wa usafiri.
Alisema wanakabiliwa na ukosefu
wa jengo la ofisi ambayo ingesaidia kuelekeza wananchi wengi kupeleka kero na
malalamiko kwa urahisi na kuomba serikali iwapatie jengo la kufanyia shughuli
hiyo,ambayo inapelekea abiria wengi kupoteza haki zao za msingi hasa ajali
zinapotokea.
Aidha katika kongamano hilo klabu
za wanafunzi hao walijitokeza katika uchangiaji damu wakatihuohuo Mkuu wa
Kitengo cha damu salama kigoma Juma Kiangi akiri wananchi wanapenda kuchangia damu,lakini
ukosefu wa usafiri wanashindwa kuwafikia wakazi waishio vijijini na nje ya mji.
Mwisho.
Na Magreth Magosso,Kigoma
MWITO umetolewa kwa viongozi wa madhehebu
mbalimbali ya dini Nchini ,waongeze maombi kwa Rais John Magufuli kwa kuwa kitendo cha kubana mianya ya rushwa kwa mafisadi wa uchumi si cha kubezwa bali
yanahitajika maombi ya nguvu ili kuondoa nguvu za giza zitakazoweza kumtoa
katika dira ya Serikali ya haki na uwajibikaji.
Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi
wa Shirika la Compassion Tanzania ( C I T)Agness Hotay alipokuwa akizungumza na
JamboLeo Kigoma Ujiji kwenye ziara ya ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa vyoo na majiko ya kisasa yenye
thamani zaidi ya fedha mil.700 katika vituo vya huduma kwa watoto yatima na wenye maisha
magumu kwa makanisa washirika ya Kiinjili ya humu, ambapo huwajengea uwezo wa
elimu,afya,malazi na chakula.
“kazi ya kupiga vita uovu ndani
ya serikali ni ngumu kwa rais wetu,maombi yanahitajika kwa viongozi wa dini kwa
kushirikiana na waumini wa kweli rais atashinda tusimwachie mzigo huu peke yake,rasilimali fedha ina hitaji
umakini katika matumizi ya kumpendeza mungu” alisisitiza Hotay.
Aidha aliwakumbusha viongozi wa
dini wanapopata fursa ya kuaminiwa katika usimamizi wa rasilimali watu
wahakikishe wanatoa elimu sahihi ya kiroho ili itakayomuongoa mwanadamu katika
ulimwengu wa roho ya kweli na si kutumia dini kujilimbikizia mali ilihali jamii
inanuka kwa ufakiri wa kipato,afya,elimu na chakula.
Aliipongeza serikali ya Magufuli
kwa kuwapa fursa makanisa ya kipentekoste 15 ya kigoma na mikoa mingine
kwa kuwahudumia wananchi katika changamoto
mbalimbali zinazowakabili hasa katika sekta ya afya,elimu,malazi,chakula na
usalama pamoja na kulinda haki za mtoto kwa kuimarisha ulinzi dhidi ya wahalifu
wanaowanyanyasa watoto .
Kwa upande wa mwenyekiti wa watenda
kazi Cluster ya kigoma (C I T) Robert Chamungu aliongeza kwa kusema kutokana na
mahusiano mema na serikali ya awamu ya tano kupitia makanisa hayo wanatarajia
kujenga nyumba 11 kwa watoto yatima wenye uhitaji wa hilo,ikiwa ni sehemu ya kumcha
mungu kwa vitendona kusisitiza hawabagui dini ya mtoto wanalenga kulind maslai
ya yatima na wenye maisha duni sana.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269