Hatimaye na baada ya muda mrefu wa
vutanikuvute ya mazungumzo ya kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo, serikali na upande wa upinzani zimetiliana saini ya kumaliza hali
ya mchafukoge nchini.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, pande mbili zitaunda
serikali ya mseto kuelekea uchaguzi wa rais utakaofanyika mwezi April
mwaka 2018, kama ambavyo Rais Kabila ataendelea kuwa rais hadi wakati
huo.
Hii ni katika hali ambayo mrengo wa mzee Étienne Tshisekedi umepinga
vikali kuafiki mpango huo, huku ukisisitiza juu ya kuondoka madarakani
Rais Kabila kufikia mwishoni mwa mwezi Disemba mwaka huu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269