.

WATU KADHAA WAUAWA KATIKA MAPIGANO YA KIKABILA MKOANI TANGANYIKA, KONGO DR

Oct 18, 2016

Mapigano yameripotiwa kujiri katika mkoa wa Tanganyika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kiongozi wa eneo la Kabalo katika mkoa huo wa Tanganyika bwana Hubert Kanza Vumba amesema kuwa, watu 16 wameuawa katika mapigano hayo ya kikabila mkoani hapo. Kwa mujibu wa Vumba, mapigano hayo yamejiri katika kijiji cha Kabumba eneo hilo la Kabalo, mkoani Tanganyika, mashariki mwa nchi hiyo.
Mkoa wa Tanganyika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Amebainisha kwamba kufuatia mauaji hayo, yeye na wajumbe wa kamati ya amani wamewasili eneo la tukio kwa lengo la kurejesha usalama. Hubert Kanza Vumba amesema kuwa, mapigano hayo yaliyoibuka tangu siku ya Jumamosi, yameendelea hadi leo. Aidha amesisitiza kuwa wakazi wa eneo la Kabalo wamepatwa na wasi wasi wa maisha yao na hivyo wamekimbilia katika ofisi za serikali. Inafaa kuashiria kuwa, kwa mara kadhaa, mapigano ya kikabila yamekuwa yakijiri katika eneo hilo la Kabalo mkoani Tanganyika na kusababisha mauaji ya watu.
Moja ya watu wa makabila yanayoishi mkoa huo
Licha ya kwamba hivi karibuni viongozi wa makabila mawili hasimu yanayoishi eneo hilo walikubaliana kuishi pamoja kwa amani, bado mapigano yamekuwa yakijiri mara kwa mara baina yao.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช