Kufuatia
changamoto ya uhaba wa ajira hususani kwa vijana nchini, wametakiwa
kuwa wabunifu na watafutaji wa fursa za kujiajiri badala ya kuilalamikia
serikali kuwa haitatui changamoto hiyo kwa muda mrefu.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na
Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel wakati akizungumza katika Kongamano
la Vijana lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na
maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika
jana jijini Dar es Salaam kuelekea sherehe za maadhimisho ya wiki ya
Umoja Mataifa, amesema vijana inabidi wawajibike katika kuleta maendeleo
ya uchumi kwenye jamii inayowazunguka na Taifa kwa ujumla.
Pia
amesema vijana waache kuhoji serikali kuwa inawafanyia nini badala yake
wawe wazalendo kwa kuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya Taifa lao.
Katibu
Mkuu wa wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante
Ole Gabriel akifungua kongamano la vijana kutoka shule na vyuo
mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika
uchumi na maendeleo ya jamii" kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa
Mataifa lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini
Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere
(JNICC). (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
"Tuna
kazi kubwa ya kujenga fikra za vijana kwamba ili kufanikiwa katika
maisha siyo lazima kuajiriwa, vijana wengi ukiwahoji wanakwambia
changamoto kubwa wanayoikabili ni ukosefu wa ajira. Lakini wanasahau
kuwa changamoto zipo nyingi zinazowakabili," amesema.
Prof.
Ole Gabriel amezitaja changamoto nne zinazokabili vijana ambazo
zinasababisha washindwe kujiajiri au kushindwa kujiendeleza pindi
wanapojiajiri kuwa ni, ukosefu wa fikra kutokana kwamba wengi
hawaziruhusu fikra zao kubuni mbinu za kujiajiri. Changamoto nyingine
aliyoitaja ni vijana kukosa uelewa, mbinu na ubunifu wa kuongeza thamani
ya shughuli wanazofanya.
Changamoto
nyingine aliyoitaja ni mfumo mbovu na usio rafiki kwa vijana hasa
mifumo duni ya upatikanaji mitaji na masoko, hususani katika kipindi
hiki ambacho kuna wimbi kubwa la vijana wasio na ajira.
Katibu
Mkuu wa wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Prof. Elisante
Ole Gabriel akisisitiza jambo kwa vijana walioshiriki kwenye kongamano
hilo.
Ameshauri
kuwa "Hivi sasa kuna elimu ya ujasiriamali lakini niseme tu
haitomsaidia kijana kujikwamua sababu hutoa elimu ya uzalishaji pekee.
Ili kijana afanikiwe na ujasiriamali, kwanza inabidi apewe elimu ya
kufanya utafiti wa bidhaa inayohitajika kwa kipindi husika, akishajua
bidhaa hitajika ndipo afanye uzalishaji kisha hatua ya mwisho kutafuta
masoko ambayo tayari ameshayafanyia uchunguzi."
Pia
ameshauri vijana kuwekeza katika biashara kilimo kwa kuwa ndiyo sekta
pekee yenye fursa ya kutoa ajira kwa wingi kwa kuwa imeajiri asilimia 84
ya vijana.
"Tanzania
ina vijana zaidi ya milioni 16.2 ni sawa na asilimia 70 ya watanzania,
waliofanikiwa kuajiriwa katika sekta binafsi ni milioni 1, waliojiajiri
milioni 1.1 waliopo katika sekta ya umma ni 18,8000 na katika sekta ya
kilimo wapo vijana milioni 13.2 na bado nafasi zipo katika sekta hiyo,"
amesema.
Mwakilishi
kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), Annamarie Kiaga akizungumza
machache kwenye kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali
nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na
maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika
jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa
Julius Nyerere (JNICC).
Hata
hivyo, Prof. Gabriel amewaasa vijana kutotumia utandawazi vibaya hasa
mitandao ya kijamii kutokana kwamba imekuwa sababu ya vijana wengi
kutokuwa na maadili.
"Utandawazi
unabomoa uwezo wenu wa kufikiri, zamani vijana walikuwa wanakimbilia
kuwekeza katika sekta ya kilimo ila sasa kutokana na utandawazi
wanakimbilia kutafuta ajira hata kama fursa hakuna," amesema na
kuongeza.
"Msipoangalia
miaka michache ijayo tutakuwa watu wa teknolojia na mitandao. Maadili
mema tuliyojengewa yatapotea kwa sababu ya kufikiri kwamba mitindo ya
kimaisha kutoka nje ndiyo inafaa kuliko ya kwetu, inabidi turudishe yale
maadili ya zamani sababu nchi yoyote isiyokuwa na maadili, tamaduni
imeparanganyika na haina maendeleo," amesema.
Mwakilishi
kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), Annamarie Kiaga akizungumza kwa
niaba ya UN amesema kuwa shirika hilo litahakikisha linawezesha vijana
kushiriki katika maendeleo ya uchumi kwa kuwainua kiuchumi pamoja na
kutoa elimu ya namna ya kujiajiri.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine
Mushy akizungumza jambo kwenye kongamano la vijana kutoka shule na vyuo
mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika
uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na
kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa
kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mbunifu
wa mavazi Johari Sadiq akizungumzia jitihada, changamoto, fursa na
mafanikio aliyoyapata katika yake ajira binafsi kama mtoto wa kike,
kwenye kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini
lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya
jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini
Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere
(JNICC).
MC
maarufu nchini ambaye pia ni Mhamasishaji Ujasiriamali, Anthony Luvanda
akizungumzia ajira yake binafsi na mafanikio aliyonayo kwenye kongamano
la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu
ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa
na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika
ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mwezeshaji
ambaye ni Mjasiriamali kijana Stella Imma, akizungumza kwenye kongamano
la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini kuelekea maadhimisho
ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana
katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa
(UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa
kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mshauri
na Mkufunzi wa Ujasiriamali/Biashara wa Program ya anzisha na imarisha
biashara yako (SIYB) akitoa hamasa kwa vijana kutoka shule mbalimbali na
vyuo waliohudhuria kongamano la vijana kuelekea maadhimisho ya wiki ya
Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika
uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na
kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa
kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mwanafunzi
Matilda Moses wa kidato cha pili kutoka shule ya sekondari ya Gerezani
akimuuliza swali Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) juu ya kusimamia
maadili ya Kitanzania na kuwaelimisha wazazi namna bora ya kusimamia
malezi ya watoto wao jijini Dar es salaam wakati wa kongamano la vijana
kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini lililoandaliwa na Shirika Umoja
wa Mataifa linalishughulikia Maendeleo (UNDP).
Pichani
juu na chini vijana pamoja na wanafunzi kutoka shule mbalimbali
wakiuliza maswali kwenye kongamano la vijana kuelekea maadhimisho ya
wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana
katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa
(UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa
kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine
Mushy (wa tatu kulia) akifurahi jambo kwenye kongamano la vijana
kuelekea wiki ya maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba
kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii"
lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es
Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mwezeshaji
MC Anthony Luvanda akifurahi jambo kwenye kongamano la vijana kuelekea
maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu
wa vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja
wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa
mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine
Mushy akiwatambulisha baadhi maafisa wa wizara hiyo waliochini ya idara
yake ambao ni vijana na wamepata nafasi ya ajira serikalini na kuwasifia
kwamba ni wachapakazi na hodari katika vitengo vyao wakati wa kongamano
la vijana kuelekea wiki ya maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa
lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya
jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini
Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere
(JNICC).
Vijana
wakiwa wamejipanga huku wakishikilia mabango ya Malengo ya Maendeleo
Endelevu (SDGs) kwenye kongamano la vijana kuelekea maadhimisho ya wiki
ya Umoja wa Mataifa lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika
uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na
kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa
kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Mkurugenzi
wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje,
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Celestine
Mushy akiwapiga msasa vijana kuhusiana na Malengo ya Dunia kwenye
kongamano la vijana kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa
lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika uchumi na maendeleo ya
jamii" lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini
Dar es Salaam katika kumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere
(JNICC).
Picha ya pamoja.
Pichani
juu na chini ni Sehemu ya wanafunzi wa shule mbalimbali na vyuo vikuu
walioshiriki kongamano la vijana lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa
vijana katika uchumi na maendeleo ya jamii" lililoandaliwa na Umoja wa
Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini Dar es Salaam katika kumbi wa
mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC).
Baadhi
ya maafisa wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Wizara ya Mambo
ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa katika
picha ya pamoja wakati wa kongamano la vijana kutoka shule na vyuo
mbalimbali nchini lililobeba kauli mbiu ya "Wajibu wa vijana katika
uchumi na maendeleo ya jamii" kuelekea maadhimisho ya wiki ya Umoja wa
Mataifa lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN) na kufanyika jana jijini
Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere
(JNICC).
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269