Wananchi wa matabaka mbali mbali Iran
wakiwemo wanachuo na wanafunzi leo Tarehe 13 Aban inayosadifiana na
Novemba 3 wameandamana mjini Tehran na kote nchini Iran ya Kiislamu na
kuonyesha uewepo mpana wa ujumbe wa kweli na wenye taathira wa Mapinduzi
ya Kiislamu dhidi ya madola ya Kiistikbari hasa Marekani.
Maandamano ya Siku ya Kitaifa ya Kupambana na Uistikbari wa
Kimataifa yamefanyika kote nchini leo Alhamisi na kuonyesha umoja baina
ya kizazi cha zamani na kizazi kipya na wote kwa sauti moja wameonyesha
kuchukizwa na uistikbari wa kimataifa kwa kupiga nara za 'Mauti kwa
Marekani' na 'Mauti kwa Israel'.
Maandamano hayo yameonysha kuwa, watu wa Iran, sawa na miaka 37
iliyopita, wanafahamu kikamilifu kuhusu njama za Marekani dhidi ya Iran
na kwamba hawaliamini dola hilo la kibeberu. Tarehe 4 Novemba mwaka
1979, wanafunzi wa Iran katika kulalamikia njama za Marekani dhidi ya
Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran walivamia na kuzingira 'Pango la Ujasusi'
(Ubalozi wa Marekani) mjini Tehran kwa lengo la kuzuia dola hilo la
kibeberu kufikia malengo yake haramu dhidi ya mapinduzi machanga
yaliyokuwa yamefikia ushindi Februari mwaka huo.
Nyaraka zilizofichuliwa katika Pango la Ujasusi zilithibitisha kuwepo uadui na njama kubwa za Marekani dhidi ya taifa la Iran.
Njama hizo zinaendelea hadi leo kwa njia mbali mbali na hata baada
ya vijana wanamapinduzi na wabunifu kuteka Pango la Ujasusi, lakini adui
angali anaendeleza njama zake. Kwa msingi huo kizazi cha vijana
wanamapinduzi hivi leo kina ufahamu wa kina zaidi kuhusu uadui wa
Marekani dhidi ya Iran na hivyo vijana hao wamechukua hatua za kuzuia
njama zaidi za dola hilo la kibeberu.
Ubunifu wa vijana wa Iran katika kuteka Pango la Ujasusi mjini Tehran
ulikuwa na taathira kubwa kiasi cha Imam Khomeini MA kuutaja ubunifu
huo kuwa, 'Mapinduzi ya Pili'.
Kauli hii ya Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilitokana na
kina cha njama na ukhabithi wa Marekani wakati wa Ushindi wa Mapinduzi
ya Kiislamu na baada ya hapo. Punde baada ya ushindi wa Mapinduzi ya
Kiislamu, dola la kiistikbari la Marekani lilianza kutekeleza njama
dhidi ya mapinduzi haya ya watu wa Iran. Lakini kutokana na uangalifu
pamoja na mwamko wa watu wa Iran, njama hizo zilisambaratishwa.
Kama alivyosema Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya
Kiislamu, kutekwa Pango la Ujasusi kulikuwa ni jibu muafaka la wananchi
dhidi ya uadui wa dola la Marekani linalojitakia makuu ambalo kwa miaka
mingi lilikuwa likipora utajiri wa Iran lakini mikono yake ikakatwa
kufuatia ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Kwa maneneo mengine ni kuwa, kutekwa Pango la Ujasusi la Marekani
Tehran kulikuwa ni mwisho wa satwa yake nchini hapa. Jambo hilo
linaonyesha wazi kwamba madola makubwa kama Marekani yatafeli katika
njama zao dhidi ya Iran. Kuendelea uadui wa serikali mbali mbali za
Marekani dhidi ya Iran kunatokana na kuendelea moyo wa hasira na chuki
dhidi ya Marekani miongoni mwa wananchi wanamapinduzi wa Iran.
Kusimama kidete Imam Khomeini MA mbele ya Marekani na pia kauli yake
aliposema, "Pigeni Makelele Mnazoweza Dhidi ya Marekani" ni ishara ya
ufahamu wake wa kina kuhusu uadui wa Marekani dhidi ya Iran na hilo
limethibitika katika historia.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Khamenei amesema
kuvunja Marekani ahadi zake katika mapatano ya nyuklia ni misdaki ya
wazi ya kuendele uadui wake dhidi ya Iran. Amesisitiza kuwa, njia muhimu
zaidi ya kustawi nchi si katika kufanya mazungumzo au kujikurubisha na
Marekani bali ni kutegemea uwezo wa vijana ndani ya nchi na kuwa macho
mbele ya sera hasimu za Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Katika taarifa ya mwisho wa maandamano ya Tarehe 13 Aban Alhamisi
hii, washiriki wamesema hatua ya wananchi wa Iran ya kupinga dhulma na
uistikbari imetokana na misingi ya Qur'ani Tukufu na mtazamo wa
kimantiki. Aidha washiriki wamesema wataendelea na mkondo huo kwa
kufuata miongozo ya Imam Khomeini MA na pia kwa kutii amri zenye hekima
za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu mbele ya uistikbari wa
kimataifa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269