.

GARI LA KUBEBEA MAJENEZA LA KIPEKEE LAINGIA NCHINI

Jul 31, 2015

 IMG_0469
Pichani juu na chini ni muonekano wa Gari maalum la kukodisha kwa ajili ya shughuli za kubebea majeneza katika misiba limeingia nchini.
Kwa wanaohitaji kukodi kwa shughuli za misiba wanaweza kuwasiliana kupitia barua pepe kiwiaadavidson@hotmail.com au simu namba +255 715 213213, +255 713 616606 na +255 784616606
IMG_0459 IMG_0481
Muonekano wa ndani sehemu maalum linapowekwa jeneza.
IMG_0477

RAIS YOWERI MUSEVEN AFUNGUA MKUTANO WA MARAIS WASTAAFU KATIKA HOTELI YA SERENA JIJINI DAR ES SALAAM

????????????????????????????????????
Rais Yoweri Museveni wa Uganda akifungua rasmi mkutano wa Marais wastaafu wa Afrka AFRICA LEADERSHIP FORUM unaofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam Mkutano huo unaojumuisha marais wastaafu Benjamin Mkapa wa Tanzania , Olusegun Obasanjo wa Nigeria, Hifikepunye Lucas Pohamba wa Namibia, Festus Mogaye wa Botswana, Bakili Muluzi wa Malawi na Jerry Rowlings wa Ghana unajadili masuala mbalimbali ya maendeleo katika bara la Afrika na Changamoto zinazokabili barahilo na umeandaliwa na Taasisi ya Uongozi Institute.
????????????????????????????????????
Marais wastaafu Bakili Muluzi wa Malawi kulia na Jerry Rawlings wa Ghana wakiwa katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo kushoto na Salim Ahmed Salim Katibu Mkuu Mstaafu wa AU na Waziri mkuu Mstaafu wa Tanzania wakiwa katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Baadhi ya waalikwa kutoka taasisi mbalimbali wakiwa katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Gavana wa Benki Kuu Prof. Beno Ndulu wa tatu kutoka kulia na wageni mbalimbali wakihudhuria katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Marais wastaafu kutoka kushoto ni Hifikepunye Lucas Pohamba wa Namibia, Benjamin Mkapa wa Tanzania na Festus Mogaye wa Botswana wakifuatilia mkutano huo.
????????????????????????????????????
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel wa pili kutoka kulia pamoja na watendaji wa taasisi mbalimbali wakifuatilia mkutano huo.
????????????????????????????????????
Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa akitoa mada katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mh. Rais Yoweri Museveni wa Uganda kulia akiwa katika mkutano huo pamoja na marais wastaafu kushoto ni Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo.

MAFISADI WAHAHA KUMZUIA NAPE MTAMA


Ikiwa imebaki siku moja kufanyika kwa kura za maoni Ubunge wa Jimbo la Mtama ,kumekuwa na michezo ya kumchafua kisiasa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye ni mmoja wa wagombea wenye nguvu kubwa kwa jimbo la Mtama.
Huku hujuma hizo zikihusishwa na mikakati ya mafisadi kumzuia Nape, ambaye amekuwa mwiba mkali sana kwa mafisadi kwa miaka sasa, ametajwa aliyekuwa akitafuta kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM ambaye jina lake lilikatwa katika hatua za awali kuhusika na njama hizo chafu.
Taarifa zilizosambazwa jioni hii kwenye mitandao mbalimbali zilidai Nape amehojiwa na Takukuru Lindi kwa Masaa matano wakati haikuwa kweli.
Kamanda wa PCCB mkoa wa Lindi S. Chami amethibitisha kuwa Nape Nnauye alikuwa ametoa pesa benki kwa ajili ya malipo ya mawakala na si wajumbe kama ilivyovumishwa.
"
CORRECTION: After questioning, it turned out that the money Nape Nnauye withdrew  was for agents, not delegates, Lindi  PCCB  boss S. Chami clarifies Friday." 


Nape amesema anajua mafisadi wanahaha kumchafua hata kufikia hatua ya kutumia baadhi ya watumishi wa serikali na mitandao ya kijamii lakini hawatofanikiwa.


" Najua wanaogopa nikiingia bungeni itakuwa kiama chao, sasa wanahaha kunizuia. Wametumia pesa na ghiliba za kila namna wanashindwa na watashindwa vibaya kesho. Mungu mkubwa" alikaririwa Nape

ALEX MSAMA:MAANDALIZI YA UZINDUZI WA ALBAM YA BONNY MWAITEJE YAMEKAMILIKA

????????????????????????????????????
Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu Uzinduzi wa albam ya muimbaji wa nyimbo za injili Bonny Mwaiteje utakaofanyika jumapili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, uzinduzi huo utashirikisha mwimbaji wa nyimbo za kutoka Zambia Ephraim Sekereti Faustine Munishi pia atashiriki kwenye uzinduzi huo na waimbaji wengine wengi kutoka hapa nchini. Fedha zitakazopatikana katika uzinduzi huo zitanunua baiskeli kwa ajili ya kuwapatia walemavu katika mikoa ya Ruvuma na Morogoro ambayo haikupata katika mgao wa kwanza na pia zitanunua Chakula kwa ajili ya vituo vya watoto yatima.

SIMBA YAIKANDIKA 4-0 BLACK SAILOR MJINI ZANZIBAR KATIKA MECHI YA KIRAFIKI

Kikosi cha Timu ya Black Sailor iliopanda daraja mwaka huu kucheza Ligi Kuu ya Zanzibar kwa Msimu wa mwaka 2015/2016, ilikubali kupigo cha mabao 4-0 dhidi ya timu ya Simba katika mchezo wa kirafiki uliofanyika usiku huu katika uwanja wa Amaan Zanzibar. 
Kikosi cha Simba kilichotoa kipigo kwa Timu ya Black Sailor uwanja wa Amani usiku huu Simba ikiwa Zanzibar kwa michezo ya kirafiki kuimarisha Kikosi chake kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania. 
       Jopo la Makocha wa timu ya Simba wakifuatilia mchezo huo wa kirafiki na timu ya Black Sailor
Mchezaji wa timu ya Simba akikokota mpira akijiandaa kumpita beki wa timu ya Black Sailor, wakati wa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan timu ya Simba imeshinda 4--0
Mchezaji wa timu ya Black Sailor akiwapita wachezaji wa timu ya Simba katika mchezo wa kirafiki.
                    Mshambuliaji wa timu ya Simba akimpita beki wa timu ya Black Sailor

Mchezaji wa timu ya Simba Abdi Banda akiifungia timu yake bao la kwanza kwa kichwa katika mchezo huo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Amaan timu ya Simba imeshinda bao 4--0
Wachezaji wa Simba wakishangilia bao lao la kwanza lililofungwa na mchezaji Abdi Banda kwa kichwa baada ya kupigwa krosi na Khamis Kiiza, mwenye jezi namba 5
Mshambuliaji wa timu ya Simba akimpita beki wa timu ya Black Sailor wakati wa mchezo wao wa kirafiki.
              Mshambuliaji wa timu ya Simba Khamis Kiiza akimpita beki wa timu ya Black Sailor


Mshambuliaji wa timu ya Simba na Black Sailor wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar timu ya Simba imeshinda 4--0 mchezo uliofanyika usiku huu.
Mshambuliaji wa timu ya Simba akizuiya mpira huku mabeki wa timu ya Black Sailor wakijiandaa kumzuiya.
       Kipa wa timu ya Black Sailor akidaga mpira ikiwa moja ya ulio gplini kwa timu ya Black Sailor
Mshambuliaji wa timu ya Simba akiruka kiunzi cha beki wa timu ya Black Sailor wakati wa mchezo wao wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Amaan Timu ya Simba imeshinda 4--0
Goli la pili la timu ya Simba lililofungwa na mshambuliaji Ibrahim Hashim katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo wa kirafiki uliofanyika uwanja wa amaan timu ya Simba imeshunda 4--0
                           Beki wa Timu ya Black Sailor akiokoa mpira galini kwake
Mchezaji wa Simba akiwa juu akipiga kichwa golini kwa timu ya Black Sailor.
Beki wa timu ya Black Sailor akioko mpira golini kwake wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Amaan Timu ya Simba imeshinda 4-0. Picha na OthmanMapara.Blog. Zanzinews.com  

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA KIA-MERERANI, JIJINI ARUSHA

Jul 30, 2015

ma1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi wa Mji mdogo wa Mererani, wakati wa hafla ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani yenye Kilometa 26. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30, 2015. Picha na OMR
ma2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, na baadhi ya viongozi wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, wakati wa hafla fupi iliyofanyika mji mdogo wa Mererani, leo Julai 30, 2015. Picha na OMR
ma3
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, na baadhi ya viongozi wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, wakati wa hafla fupi iliyofanyika mji mdogo wa Mererani, leo Julai 30, 2015. Picha na OMR
ma4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na baadhi ya Viongozi,kwa pamoja wakikata utepe kuashiria kuzindua rasmi harakati za ujenzi wa Barabara ya Kilometa 26 ya Kia-Mererani, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika mji mdogo wa Mererani leo Julai 30, 2015. Picha na OMR
ma5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa vazi la kabila la Masai na Kiongozi wa Mila ya Laibuwanani, Kisota Lengitambi, wakati wa hafla hiyo ya uwekaji wa Jiwela Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani. leo julai 30, 2015. Picha na OMR
ma6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa makabila mawili makubwa ya Kimasai baada ya kumvisha vazi hilo. Picha na OMR
ma7
Dkt. Bilal akiagana na viongozi hao wa kabila la Masai.
ma9
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia- Mererani, leo Julai 30, 2015. Picha na OMR
ma10
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi. Picha na OMR
ma11
Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal. Picha na OMR
ma13
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, wakicheza sambamba na kinamama wa kabila la Kimasai wakati wakifurahia ngoma ya Kimasai kwenye hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, leo Mkoani Manyara. Picha na OMR
ma14
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, wakifurahia ngoma ya asili kwenye hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, leo Mkoani Manyara. Picha na OMR

KURASA ZA MBELE ZA BAADHI YA MAGAZETI YA LEO JULAI 30, 2015

ยช